MKALI wa Sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefungukia taarifa zilizozambaa mtandaoni kuwa mzazi mwenzake, Moze Iyobo ana kifaa kingine huku zikionekana picha wawili hao wakiwa wamevalia sare za jezi kwa kusema kuwa hayo mambo hayamhusu.
Aunt ambaye amezaa na Iyobo mtoto mmoja alisema kuwa hana muda wa kufuatilia mambo ya mtandaoni kwa sababu ana vitu vingi vya kufanya na siyo kumfuatilia mtu amefanya nini au anatoka na na nani kwa sababu mwisho wa siku kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
“Unajua kila siku ukikaa kwenye mitandao unasubiria nani kafanya nini, huwezi kusonga mbele hata kidogo kwa kweli hivyo kama picha imesambaa sijui nini havinihusu kabisa kama tuko sawa ndani hiyo pekee inatosha,” alisema
No comments:
Post a Comment