Njia 10 Ambazo Wanawake Hupenda Kutongoza Wanaume Bila Kujua Kama Huchukiza - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 7, 2019

Njia 10 Ambazo Wanawake Hupenda Kutongoza Wanaume Bila Kujua Kama Huchukiza



Utongozaji ni jambo ambalo hutumiwa na kila mtu yule. Kuna njia kadha wa kadha ambazo zinaweza kutumiwa kufanya mtu aingie katika mahusiano ya kudumu na yeyote yule.

So watu hutongoza vipi?



Hivi kuna kanuni zozote za kutongoza? Je kuna sheria flani ambazo watu hufuata ambazo hutumika? Ama huwa inakuja tu yenyewe wakati wa kutongoza? Kwa wanawake, kutongoza si jambo la lazima, kwa sababu kuna asilimia kubwa ya mwanaume ambao huanzisha kutongoza. Lakini wakati mwingine inatokea kuwa mwanamke anapaswa kuchukua hatua ya kuanza kumtongoza mwanaume.

Wakati ambapo mwanamke anahisi ya kuwa hapati atenshen inayotakikana, anaweza kuamua kuchukua hatua nzito ambayo inaweza kufanya kazi ama kutoweza, kwa lengo moja la kuhakikisha kuwa anaonekana na mwanaume. Mara nyingi hatua hizi huwa zinatokana na maonyesho ya runinga au filamu.

Ok. kuna njia kadha wa kadha ambazo mwanamke hutumia kumtongoza mwanaume. Zile ambazo hujulikana sana ni kama:


kuangalia macho


kumnunulia mwanaume kinywaji 


kumsifu


kutabasamu


nk


Hii ni baadhi ya kutongoza ambakwo mara nyingi hufanya kazi. Lakini kuna baadhi ya wanawake ambao hawaridhiki na hatua hizi na hujaribu kutafuta mbinu nyingine ambazo wanaamini ya kuwa zinaweza kumsahiwishi na kumtia box mwanaume, baadhi ya mbinu hizi huwa sawa na nyingine huwa potoshi.

Je ni mbinu gani za kutongoza ambazo wanaume huchukizwa?

Mbinu hizi awali zilikuwa zikitumika kwa njia rahisi sana lakini kwa sasa zimepitwa na wakati na huashiria mambo tofauti. Ushauri kwa mwanamke ni kuwa kama iwapo unataka mahusiano ya kufaana na mwanamke basi usiwahi kutumia kamwe hatua hizi.

1. Kuyapanga matiti yako

Hii inakubalika kutumika kama ni dharura. Kawaida hakukosekani sehemu ya mapumziko ya mwanamke iwapo anataka kuyatandaza ama kuyatengeneza matiti yake.

Kuyatengeneza matiti yako yakae vizuri hadharani inaonyesha kukosa ustaarabu na kukosa heshima kijamii. Si hivyo pekee bali pia wanaume hawavutiwi kamwe na hatua kama hii. Ukianza kuyatandaza matiti yako huku na kule kunawafanya wanaume kujihisi kuwa na aibu kimpango. 

2. Kuramba midomo yako kiushawishi

Kuramba midomo yako kwa njia ya kuifanya iingiwe na unyevu inakubalika. Lakini kuramba midomo yako kana kwamba mwanaume ulietoka naye deti ni ice cream ambayo unataka kuila inaogofya. Mwanzo kwa mwanamke ukiwa unaramba midomo yako kwa ushawishi kunaweza kumfanya aongope kuwa unaweza kumla wakati ambapo mtakuwa wawili pekeenu. Ok, najua kuramba midomo huwa kunaleta hisia za mapenzi lakini haipaswi kufanywa hivyo sehemu za hadhira.

3. Kuomba msaada wakati ambapo hauhitajiki

Kuna tabia ambayo wanawake hupenda kuitumia mara kwa mara, tabia ya kufanya kitu kuwa kina dharura na ambacho anahitaji msaada wa haraka kutoka kwa mwanaume. Jambo la rahisi analifanya kuonekana zito.

Wanaume wanapenda wanawake ambao wanapenda kujitegemea wao wenyewe, na ambao hawaonyeshi pupa ya kutaka usaidizi hata kama wanataka.

4. Kurusha nywele kupindukia

Mwanamke anapaswa kuzirusha nywele zake nyuma wakati ambapo anamtongoza mwanaume lakini haufai kuzidisha. Kila kitu kina kiasi flani. Hivyo kabla kuzirusha nywele zako mara kwa mara hakikisha ya kuwa hazitorusha chembechembe yeyote za uchafu ama kutoa harufu ambayo inaashiria hazijaoshwa kwa muda.

5. Michezo ya kumfinya, kumgonga, kumpiga kofi nk

Je wewe huona kuwa kufanya hivyo ni furaha? Kwa mwanaume ni LA, ni vile tu hawapendi kusema kwa nguvu. Lakini ukweli ni kuwa wanaume hawapendi kuumizwa na kugongwa haswa sehemu za hadharani. Uchungu ni ule ule hata hauchagui unamuumiza nani. Hivyo tabia kama hiyo haiwapendezi kamwe wanaume.

6. Kujishika kope zako

Huwa inaonekana vizuri wakati ambapo unafikiria jambo kama hili, lakini wanaume wanapoteza umakini wao kwa mwanamke iwapo kila mara atakuwa akizishika kope zake. Hii ni mbinu ya kutumiwa mara moja na wala si kila wakati. Mara nyingi itaoneka kwamba kuna kitu kimekuingia machoni mwako, na mwanaume hawezi kujizuia ila kujaribu kukupuliza ili kusaidia kutoa huo uchafu. Mara nyingi hatua hii inafanya mwanaume apoteze umakini kwako kwa sababu ya hilo jambo.

7. Kuandama wanaume kila mahali

Wewe umekuwa mtu mkubwa hivyo tabia za kufuata na kuandama watu kila mahali si mpango. Unafaa kuacha kuandamana na wanaume kila mahali na uanze kuzungumza kile ambacho kiko alikini mwako. Fahamu ya kuwa tabia ya kuandamana mtu kila mahali huwezi kutofautisha iwapo umependezwa ama una tabia za kunyatia.

8. Kula chakula kutoka kwa sahani ya mwanaume

Hii ni tabia ambayo kuna wanawake ambao wanaipenda sana. Mbona usingojee kama mwanaume ataagiza kula kwa sahani yake? Kawaida kuna kitu ambacho hakitaonekana sawa iwapo utarukia kuanza kula katika sahani ya mwanaume. Kama umekuwa ukideti na mwanaume kwa muda mrefu hio ni sawa. Lakini iwapo umeanza kujuana na mtu hivi karibuni na kuanza tabia kama hii humchukiza mwanaume hapo hapo.

9. Kujaribu kuongea kuhusu vitu mwanaume anapenda halafu kushindwa kustahimili

Wanaume wengi huona ya kuwa inakaa raha iwapo kuna maslahi ambayo anagawa sawa na mwanamke. Lakini iwapo mwanamke ataiga na kujifanya ya kuwa anagawa interest moja na mwanaume huwa kawaida atagundulika. Mwanaume anapenda uulize na kujua vitu anavyopenda. Hawataki uanze kutoa ujuzi na ujanja wote kuhusu jambo fulani bila wewe mwenyewe kujua chochote ambacho unaongea.

10. Kulalamika kihatia

Wanawake kulalamika kihatia huwa ni jambo zuri la kuweza kuteka atenshen kutoka kwa mwanaume, lakini kwa mwanaume anajua hio ni mbinu ambayo mwanamke anaitumia kama mchezo wa kuichanganya akili yake, Hata kama ulikuwa unataka atenshen ndogo kutoka kwake, mwanaume ataona kwamba umefanya hivyo maksudi kwa ajili yao, So tabia kama hio inaweza kuharibu siku yao, na pia wewe iwapo hawaingiliana na ujanja wako.

Hivyo kama kweli unamtaka mwanamke, tungekushauri uwe mkweli na mwenye mwelekeo. Kama mwanaume hakuvutiwa kwako, ni vizuri uchunguze chanzo chake badala ya wewe kujaribu kutongoza kwa njia ambayo inaenda mrama.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages