Fahamu Dalili Za Kuchokwa Na Mpenzi Wako - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 7, 2019

Fahamu Dalili Za Kuchokwa Na Mpenzi Wako

Watu wengi wamekuwa wakilia katika mapenzi na kuumizwa sana, wanafikia hatua mpaka ya mwisho mwenzi wako anapoamua kutafuta mtu mwingine ndio na wewe unashtuka kuwa kumbe huyu mtu amekuchoka, aina haja ya kuangaika hivyo zipo dalili za mwanzo kabisa ambazo zinaweza kukuonyesha kuwa hapa ni muda wa kubebab virago vyako na kuondoka tu,dalili hizo ni pamoja na ;

1.Hakupigii simu mpaka umpigie

mawasiliano ni moja ya vitu ambavyo vinajenga mahusiano ya watu wawili kwa nguvu zaidi, haijalishi kama mko mbali au mnakaa pamoja, kumkumbuka mpenzi wako na kumoigia au kumtumia meseji kunaonyesha ni jinsi gani unamuhitaji mwezi wako,lakini mara mwenzi wako anapoanza kukuchoka basi mawasiliano huanza kupungua kabisa, hakupigii wala kutuma meseji mpaka umuanze kama hauna salio basi ndio imetoka , na bado ukimtafuta hakosi kulalamika.

2.Malumbano ya mara kwa mara

mwenzi wako anapoanza kukuchoka basi uanza kuzua jambo dogo likawa kubwa ilimrdai tu ugomvi utokee, kama mwanzo hakuwa na tabia hiyo basi ujue wazi kuwa majibizano na ugomvi wa mara kwa mara ufanya watu wachokane na hatimaye kuvunja amani kabisa.

3.Ukimpigia simu usiku atakwambia anataka kulala lakini ukipiga baadae unakuta simu inatumika,

watu wa aina hii wanatabia ya kukukwepa , siku zote hakusi sababu ya kutokupokea simu yako au kuongea nae, utashangaa ukipiga anakambia anataka kulala au yuko busy , lakini ukijaribu kupiga baadae utaona simu inatumika , ukiona hivyo anza kuongoza njia.

4,Mpenzi wako hana muda na wewe

Ule muda mliokuwa mkikaa pamoja hapo tena kati yenu,atatafuta sababu ya kuwa busy  na biashara au kazi zake ili tu aweze kukukwepa kabisa, lakini kwa mtu anaekupenda hawezi kukosa muda kabisa na wewe, watu huwa wanasema “no one is busy but its a matter of priorities”,  inatakiwa atenge muda wa kazi zake na muda wa kukaa na wewe pia.

5.Kupoteza hamu ya kufanya mapenzi na wewe

hapa ndipo usaliti uanpoanzia, mwenzi wako anapoanza kuoneka kupoteza mood ya kuwa faragha na wewe ilo ni tatizo kubwa, inawezekana kuna kitu hakiko sawa kwako, lakini kama unajitahidi kuchunguza kutoka kwake na badohauna shida mnapokuwa chumbani, basi ujue kuna shida inataka kutokea na iyo ni dalili.

Watu wengi tumekuwa tukisumbuliwa na mapenzi, mara nyingine huwa tunahisi kuwa wale tulionao katika mahusiano hatuwezi kuwaacha kwa sababu tunaogopa kuumia, sio kweli unapoanza kuona dalili hizo ni bora kujiengua mapema kabla haujaumia zaidi.Mtu yeyote uliyenae katika mapenzi na akawa anakusumbua jua kuwa huyo sio wako ,mwache aende zake.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages