Wanaume wengi huingiwa na mawazo na maswali mengi jinsi ya kupata girl friend. Wengi wanaingiwa na mawazo ya jinsi ya kuapproach mwanamke, bila kugusa swala la kudeti na kumfanya awe girl friend wako. Wakati mwingi wanaume hubakiwa kuingia na wasiwasi ama misongo ya mawazo kiasi cha kuwa wanapoteza kujiamini kwao hivyo kukosa kumweleza vyema mwanamke kama umempenda.
Uzuri ni kuwa kuna njia tofauti tofauti za kukabiliana na jinamizi hili. Haswa kwa wale wanaoanza kuna mambo muhimu wanayofaa kufuata. Kwanza ni kuwa ujiweke wewe mwenyewe bila kuiga mwingine, pili ni uhakikishe ya kuwa timing yako iko sawa, na tatu hakikisha ya kuwa uwe mwaminifu kwake.
Zama nami nikuonyeshe hatua za kufata upate girlfriend.
Hatua za kufanya ili upate girlfriend
1. Jitayarishe kwa changamoto
Kabla hujaingiwa na wazo la kuapproach mwanamke lazima uwe na uwezo wa kujiamini. Wanaweka wanapenda mwanaume ambaye anajiamini. Kando na kuwa kujiamini ni kigezo kinachoangaliwa na umakini kwa mwanamke, ni lazima mwanaume awe anajiamini. Kama hujui utafanya nini ili ujiamini basi usisome hatua hizi zaidi hadi ufahamu mbinu za kujiamini.
2. Tumia Sanaa Za Kutongoza
Hapa tunataka kugonga ndipo bila kuzunguka huku na kule. Kwa wale wageni wapya kwa blog hii tunapenda wasome sanaa za kutongoza ili wapate ufahamu wa hali ya juu. Hivyo kurahisisha kazi yako ya kutongoza mwanamke, tumeandaa machapisho kadhaa ambayo yanahusiana na Sanaa Za Kutongoza.
3. Makinika na mwonekano wako
Kujiweka nadhifu ni kigezo muhimu ambacho mwanamke yeyote ataangalia. Usijaribu kuapproach mwanamke iwapo unatema mdomo, unanuka makwapa ama umevalia kichafu. Kama unajishuku kwa nini wanawake wengi wanakukataa angalia vigezo hivi muhimu.
4. Tangamana
Wanawake wameumbwa tofauti na wanaume. Mwanamke huvutiwa sana na mwanaume ambaye ana tangamana na wengine. Kama unataka attention kutoka kwa mwanamke fulani, basi tangamana na wanawake wengi. Kuwa mtu mjamiifu kwa kutangamana na wanawake tofauti tofauti. Hii itakufanya wewe kumvutia mwanamke yeyote ambaye amevutiwa na wewe.
5. Angalia kwa mtandao
Kama umeamini ya kuwa mitindo ya zamani ya kutafuta mwanamke haitafaulu, basi kuna mbinu nyingine ambayo sikuhizi inatumika sana, nayo ni kutafuta mwanamke kwa mitandao ya kijamii.
Wanaume wengi hutumia mbinu hii ya kufukuzia mwanamke kwa sababu hawataki njia ndefu za kutangamana na watu ama kujishughulisha na mwonekano wao hadi siku ambapo watakutana na mwanamke. Uzuri wa kutumia mitandao ya kijamii ni mingi sana hivyo inakupa wewe nafasi rahisi ya kumpata yule ambaye anakufaa.
6. Onekana nadhifu online
Kama umeamua kutafuta girlfriend online basi ni muhimu ujue jinsi ya kujiweka uvutie online. Kulingana na Derek Rake, mwanzilishi wa programu ya 'Online Dating Playbook', anadai ya kuwa iwapo unataka kuvutia wanawake kwa mitandao ya kijamii basi lazima uweke profile pic ya kuvutia, post unazozirusha ziwe za mnato, na pia kutangamana na wanawake tofauti tofauti ili ujue tabia zao. Pia ni muhimu kufanya video chat na mwanamke kabla kuchukua hatua yeyote ya kutaka kukutana naye.
7. Ijue sehemu utakayompeleka
Iwe unamtoa out mwanamke uliyempata online ama offline, lazima ujue sehemu ambayo utamtoa out. Sehemu ambayo unachagua kumtoa out mwanamke mara ya kwanza ni muhimu zaidi kama una ajenda ya kutongoza. Sehemu nzuri ya kumtoa out mwanamke ni sehemu ya umma. Hii itaondoa majaribio ambayo unaweza kuwa nayo ambayo yanaweza kuharibu kila kitu.
8. Mtoe out kwa mara ya pili
Kama out yenu ya mara ya kwanza imefaulu, usisahau kumwambia ya kuwa ulipenda makutano yenu na ungependa muwe na kikao kingine naye. Hii itakuwa ni point kubwa umepata katika azma yako ya kumfanya kuwa girlfriend wako.
No comments:
Post a Comment