Inawezekana anafanya kazi, kutwa nzima yuko kazini, anahangaika na bosi akitoka anarudi nyumbani, anakutana na watoto ambao hata kuoga bado, hapo hajakupikia chakula kukuandalia maji ya kuoga na kukupigia nguo pasi kisha usiku unataka mechi. Kumbuka hiyo ni kila siku tangu mwanzo wa ndoa mpaka anakufa, hivi kwanini asiwe na kisirani, hembu wewe jaribu ratiba yake kwa siku moja uone kama hutachanganyikiwa.
Lakini inawezekana hata hafanyi kazi, lakini akiamka asubuhi ni mikiki mikiki ya hapo nyumbani, mbali na kazi, kuhangaika na nepi za watoto, kuhangaika na kilio cha watoto ambao hawapendi kula lakini kuna majungu ya majirani na usiku wala hapumziki, naye ni kupika, kukupasia na kukupa mechi. Kwanini asiwe na kisirani, ana raha gani ya kumfanya kucheka kama mpaka kufa anakua katika kifungo kama hicho.
Lakini wewe ratiba yako ukitoka kazini unapitia kwa marafiki, huko unatoa stress zote kabala ya kurudi nyumbani, unakutana na kila kitu kiko sawa, kimeandaliwa mpaka taulo na mafuta ya kujipaka umeandaliwa! Hivi mtu kama wewe unakua na kisirani cha nini? Sasa mwisho wa wiki badala ya kutoka na mke wako unatoka na mchepuko wako, tena unauona kama wenyewe umechangamka ukiwa nao huboreki kwakua hauna kisirani.
Unausimulia kabisa kuwa angalau ukiwa nao una amani tofauti na mkeo ambaye kila siku ni kelele. Unasahau kuwa mchepuko unakutana nao kwaajili ya starehe, kwaajili ya kuutoa out kwamba hata kama ulikua na stress lakini si unautoa out kuziondoa sasa utazionaje. Hapa ni sawa na mtu kusema si mchafu wakati mnakutania bafuni mkioga, mkeo yeye unamhukumu kusema ni mchafu wakati umemkuta shambani analima!
Mwanamke naye ni binadamu, anahitaji kupumzika na hayo maisha ya kila siku, anahitaji kubadilisha mzunguko wake wa maisha. Kutoka Kuamka-Kupika-Kufua-Kupika-Kupasi-Kitandani na angalau mara moja hata kama ni kwa mwezi ujumlishe na kutoka out. Lakini na nyie dada zangu kama mume wako hakutoi, hajali hembu chagua siku moja ya mwezi na sema leo sitapambana na Nepi nitajitoa mwenyewe, hata umuachie watoto hapo nyumbani utoke kidogo!
No comments:
Post a Comment