Mume wangu aliacha kazi miezi sita tu baada ya kuoana, kipindi hicho nilikua na ujauzito wa miezi miwili na tayari nilikua na mtoto mmoja ambaye tulizaa naye kabla ya ndoa yeye alikua mkubwa. Nilimuuliza kwanini naacha kazi na tutakula nini aliniambia kuwa kachoka kuajiriwa na kuteseka anatakla kupumzika. Aliniambia kuwa mshahara wangu unatosha kutuhudumia wote wawili anapumzika kwanza. Hakuniambia hata kama anataka kufanya Biashara, hakuniambia hata kama anataka kubadilisha kazi au kufanya kitu kingine chochote kile.
Hapo ndiyo nilianza kubeba majukumu ya kikazi, baada ya kulipwa NSSF nilitegemea labda atatafuta Biashara na kufanya, lakini pesa zake ziliisha tu kimya kimya bila mimi kujua zimeenda wapi. Alianza kubaki nyumbani, asubihi nilikua nalazimika kumka mapema kupika chakula mpaka cha mchana kisha ndiyo niende kazini. Pamoja na kukaa tu nyumbani lakini alikua hajishughulishi kwa chochote zaidi ya kuangalia TV. Nilimhudumia kwa kila kitu hata baada ya kujifungua hali ilikua ni hiyo hiyo.
Hakutafuta kazi na kila siku tulikua tukigombana kuhusiana na yeye kufanya kazi. Nililalamika mpaka nikaja kuzoea, ikawa ni kila siku naondoka nyumbani namuacha mwanaume nyumbani na binti wa kazi, nisingeweza kumnyima chakula kwakua nilikua na mtoto na kama ikitokea sijaacha pesa ya kutosha basi anachukua vitu ndani na kwenda kuuza. Hali ilikua mbaya zaidi Mama yake mzazi alipoanza kuumwa, alikuja nyumbani kwangu tukawa tunaishi wote.
Alikuja na mdogo wake wa kike amabye kipindi hicho alikua kamaliza chuo na hakua na kazi. Kumbuka tulikua tukiishi nyumba ya kupanga ya vyumba vitatu kwa maana, sebule na chumba chetu pamoja na chumba cha binti wa kazi ambacho tulikitumia kama jiko. Baada ya ndugu zake kuja ilibidi kuweka kitanda sebuleni ili bibti wakazi aweze kulala kwani chumba alichokua akilala binti wa kazi kilikua kidogo sana na kilikua na vitu vingi.
Pamoja na ndugu zake kuwa hapo nyumbani lakini mume wangu hakujali, hakua mtu wa kujishughulisha, alikua akishinda tu chumbani na nisipotoa pesa ya matumizi basi huweza kunipigia au hata kunifuata ofisini na kuniuliza “Vipi leo hatuli!” Nilimhudumia Mama yake mpaka akapona, akaondoka na kurudi kijijini, wakati wanaishi kwangu walikua na nidhamu, walijifanya kunipenda na hawakuniongelea baya lolote.
Lakini baada ya Mama mkwe kupona na kuondoka kwangu yalizuka maneno kuwa mimi namnyanyasa mume wangu, nimemlogga hataki kufanya kazi na maneno mengi kibao. Mimi nilivumilia lakini baadaye nilichoka na kuamua kumuambia mume wangu ili kuongea na ndugu zake, aliniitikia sawa tu atafanya hivyo lakini hakufanya, alikaa kimya na maneno yalizidi. Niliamua kuwapuuzia, kwakua nilijua kuwa mume wangu hawezi kunisaidia chochote niliamua kupambana.
Nilichukua mkopo kazini, kwenye SACCOS ya ofisini na kufungua Biashara, mwanzo nilitaka kumuweka mume wangu ili angalau ajishughulishe na sisi kusaidiana lakini alikataa, aliniambia kuwa hawezi kufanya bibiasharta vya kishenzi wakati yeye ni msomi. Nilinymaza kimya, nikatafuta kijana na kufungua duka la spea za Pikipiki, lilikua duka dogo tu, nilianza na mtaji wa milioni mbili.
Kwakua nilikua nasimamia vizuri na nilifahamiana na mafundi wengi wazuri nilikua nikipata wateja sana, pale nnje niliweka kama kijue, nikatafuta mafundi wawili wazuri wakawa wanatengenezea Pikipiki pale, ilikua rahisi kupata wateja kwani walikua wakija na kama kitu sina basi kijana anaenda kuwachukulia maduka mengine. Biashara ilichanganya, nilianza kujenga kimya kimya bila kumshirikisha mume wangu kwani hakutaka hata kushiriki.
Baada ya kama mwaka mmoja hivi nilifanikiwa kujenga nyumba yangu ya vyumba vitatu na sebule, hapo ndipo nilimuambia mume wangu na hapo ndipo alishtuka kuwa kumbe Biashara yangu ishakua kubwa. Alikubali kuhamia lakini cha kushangaza alileta na ndugu zake, Mama yake na wadogo zake wawili walikuja, aliniambia hawezi kuwaacha ndugu zake kwenye nyumba ya kupanga wakati kwangu kuna nyumba.
Nilikasirika sana na kutamani hata kumfukuza, lakini nilipomuambia Mama yangu mzazi alinisema sana na kuniambia nisiwe mchoyo niishi vizuri na wakwe. Walikuja kuishi kwangu na hapo ndipo nilianza kuona vituko, kwanza walikua ni wachafu, walikua wakila kila kitu wananiachia nifanye mwenyewe, hata kuosha vyombo ilikua shida na kila nikongea mume wangu anakasirika na kusema siwapendi ndugu zake. Nilinyamaza na kuvumilia nikaona kuwa ni mambo ya kupita tu.
Lakini nilipovumilia hilo na kuona kuwa siumii tena walianza maneno, kupanga kila kitu cha ndani kwangu, nikipanga tupike kitu flani wao wanabadilisha, nikipanga hiki wao ni tofauti mwanaume nikiongea ananiambia kuwa yeye ndiyo mwanaume ndani hivyo nisimpangie na kama vipi ataondoka na kuniachia nyumba yangu. bado pia nilivumilia, ila sas alikaja suala la kuleta waganga nyumbani kwangu, kila nikirudi kutoka kazini nilikuta watu ambao hawaeleweki eleweki na maharufu ya ajabu ajabu.
Hapo nilirudi tena kwa Mama, nilipomuambia basi alianza maombi, sijui nini kilitokea lakini walianza kuniambia mchawi, mume wangu akawa ananikataza kwenda nyumbani kwetu kwani kila nikienda Mama yake alikua anaumwa, walihisi mimi namloga, alikua akinipiga kila nikienda nyumbani na hata nikiongea na simu na Mama yangu, aliwachukia ndugu zangu zangu akwa ni mtu wa kutokana tu kila mara.
Siku moja nilirudi nyumbani mtoto wangu kazidiwa, alikua kadondoka shuleni na kupelekwa hospitalini lakini mume wangu alienda kumchukua na kumrudisha nyumbani, alileta watu wake wakawa wanafanya matambiko yake, nilipofika nyumbani wlainifukuza kabisa wakisema kuwa mimi ndiyo namloga mwanangu, walisema nimemtoa mtoto kafara kwaajili ya mali hivyo nisiingie mule ndani, nilijaribu kulazimishia lakini mume alinipiga sana na kuniumiza.
Nililazimishia na kuingia ndani, nilimuona mwanangu kalala yuko katika hali mbaya karibia kufa. Nilitaka kumchukua lakini walinikataza, walinishika na mganga wao na kunitoa nnje, sikukubali, niliondoka na kwenda Polisi, kwa bahati nzuri polisi walikuja na kumchukua mtoto, tukampeleka hospitalini, hali yake ilikua mbaya sana, huko hospitalini hata hawakujua nini kilikua kinamsumbua, mapigo ya moyo yalikua ni kidogo sana na alikua anaweweseka sana.
Nilihangaika na mwanangu peke yangu mpaka akanifia mikononi mwangu, alikaa hospitalini wiki mbili lakini mume wangu hakuja kumuona, yeye na ndugu zake walinisusia wakisema mimi ndiyo nimemuua mtoto, hata mazishi nilifanya mimi mwenyewe na ndugu zangu, ndugu zake waliokuja ni wale wa mbali si wale wadamu. Wote walikua wakiamini kuwa nimemloga mtoto wangu ili kupata mali, mume wangu hakutaka kuongea na mimi.
Kitu cha ajabu nikuwa hawakutaka kuondoka kwenye nyumba yangu, mume wangu alikua akikazania kuwa ile nyumba ni yetu yote na kama ni suala la talaka nidai mimi ili tugawane mali. Mwanzoni nilikataa lakini siku moja nilirudi nyumbani na kumkuta Mama yangu kadondoka, alikua kapooza upande mmoja, nilipofika Mama aliniambia mwanangu ondoka, wape kila kitu hawa watu watakuua. Nilimuuliza kwanini akaniambia Mwanangtu huna imani kama mimi, watakuua wamemuua mwanao watakuua na wewe.
Niliamua kukubaliana na mume wangu, nikadai talaka na tukagawana mali, tulitengena na kumuacha na maisha yake. Baada ya kutengana nyumba iliuzwa na kila mtu akachukua chakwake, maisha yaliendelea na baada ya mwaka mmoja nilikua na nyumba nyingine, mama yangu alipona mguu na mume wangu bado alikua anzurura mjini. Alikua kachoka, ndugu zake wamemkimbia na walianzana kushina uchawi wenye.
Alianza kuwalaumu kuwa wao ndiyo wamemsababishia kuniacha mimi, alirudi kuniomba msamaha lakini sikua tayari. Baada ya kuona kuwa simfuatilii basi alienda kwa mwanamke mwingine anaishi kwake. Hahudumii mtoto kwa chochote hata kupiga simu ni shida lakini nimeamua kuendelea na maisha yangu na nimejifunza kuwa huwezi kubeba majukumu ya mwanaume hata siku moja, jinsi unavyomdekeza na kumbebea majukumu basi ndiyo unavyomharibu.
***MWISHO
No comments:
Post a Comment