KWANINI WANAWAKE WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KIUCHUMI?
Hili ni swali la kujiuliza, kwanini mwanamke na mwanaume ambao wana mishahara au vipato sawa wanakuwa na maisha tofauti? Lawama kubwa zinapaswa kuwenda kwa jamii, jamii ndiyo ambayo imewatengeneza wanawake kwa namna hii. Jamii imemtengeneza mwanamke kwa namna kuwa anapozaliwa anapaswa kuishi na wazazi wake mpaka atakapoolewa.
Jamii imeweka kuolewa kama suala la lazima kwa mwanamke na kumtengenezea mwanamke maisha ya aina mbili tu. Maisha ya kwanza ni tangu anapozaliwa na kulelewa na wazazi wake mpaka anapoolewa na maisha ya pili ni pale anapoolewa mpaka kufa. Zaidi ya hapo mwanamke kujitegemea na kuwa na maisha yake inaonekana kama uhuni.
Hapa inaamanisha kuwa jamii inamtafsiri mwanamke kama mtu wa kulelewa kuanzia wakati anazaliwa ambapo hulelewa na wazazi wake na baada ya kuolewa ambapo hulelewa na mume wake. Imemtengeneza kuwa tegemezi na si mtu wa kujitegemea, fikra za ndoa zinakuwa kikwazo kikubwa kwa mwanamke wengi kuweza kukua kiuchumi.
Hali ni tofauti kwa upande wa wanaume, mwanaume ametengenezwa kuwa na maisha ya aina tatu. Kwanza ni kuzaliwa mpaka anapofikia hatua ya kujitegemea, hapa anakuwa analelewa kama mtoto, pili ni hatua ya kutafuta ili kuanzisha familia yake, hapa anakuwa anajilea mwenyewe na tatu ni kuoa na kuanzisha familia yake ambayo ataitunza, hapa anakuwa analea.
Hivyo kipindi cha kujiandaa kuoa kwa mwanaume ni kipindi muhimu sana cha kutafuta pesa kwaajili ya familia yake. Wakati mwanamke akisubiri kuolewa na mtu mwenye uwezo wa kifedha ambaye atayafanya maisha yake kuwa mazuri, mwanaume anatafuta pesa ili aoe mwanamke mzuri aweze kumtunza ili maisha yao yawe mazuri.
Kutokana na ukweli huo ni lazima mwanaume atafute kwa hali na mali katika kuhakikisha kua anaitengenezea familia yake maisha mazuri. Kwa mwanamke anahitaji kujitunza tu ili kuonekana mzuri na kupata mwanaume ambaye atamhudumia vizuri. Hii ndiyo maana pesa nyingi za wanawake huishia katika kununua nguo zuri, vipodozi na vitu vingine vingi ambavyo vitawafanya kuonekana wazuri na wakuvutia.
Suala hili liko wazi wala halihitaji uchunguzi wa kina. Ukitaka kuthibitisha hili angalia jirani yako au mfanyakazi mwenzako wakiume. Muuulize anapea ngapi za viatu au mashati na aliyanunua lini kisha jilinganishe na wewe.
Muulize anatumia mafuta ya aina gani na bei gani kisha jilinganishe na wewe. Matumizi ya wanawake hulenga sana katika kujihakikishia kuwa wanavutia mbele ya wanaume wakati matumizi ya wanaume ni ya kuhakikisha kuwa wanawekeza kwaajili ya familia zao.
Katika muktadha huu ni vigumu kwa wanawake kuandelea na kufanikiwa kiuchumi, mpaka wanagundua kuwa maisha yao ni yakwao wenyewe wanakuwa wameshachelewa baada ya kauchana na wanaume kadhaa bila ndoa. Katika ulimwengu wa sasa ndoa ni matokeo ya maisha na si maisha.
Ni lazima mawazo ya kusubiri mwanaume ili maisha ya anze yakome kwani anaweza asitokee. Nilazima sasa wanawake kuanza kufikiri katika maisha ambayo hayamgusi mwanaume, kuwaza kuwa na maisha yao. Mwanaume kwako anapaswa kuwa kama bonus, kitu cha zida ambacho kimetatokea wakati ukitafuta maisha yako.
Monday, February 25, 2019
KWANINI WANAWAKE WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KIUCHUMI?
Tags
# Mapenzi
Share This
About Utundu Kitandani
Mapenzi
Labels:
Mapenzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment