Zari ampa onyo kali Tanasha wa Diamond - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 11, 2019

Zari ampa onyo kali Tanasha wa Diamond




DAR ES SALAAM: Taa nyekundu! Mzazi mwenza wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwanamama mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amempa onyo mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Tanasha Donna Oketch, Gazeti la Ijumaa linakudokeza.


Zari amemuonya Tanasha akimtaka kuwa na tahadhari kubwa juu ya mpenzi wake huyo ikiwa ni siku kadhaa tangu jamaa huyo alipodaiwa kuchepuka na aliyewahi kusemekana kuwa mpenzi wake, Irene Louis ‘Lynn’.


ANAANZA HIVYOHIVYO


Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa udaku nchini Uganda anakotokea Zari, Diamond au Mondi huwa anaanza hivyohivyo kwa kudaiwa kutoka na mrembo fulani kabla ya jambo hilo kuja kuthibitika baadaye.


Zari alikuwa mwandani wa Diamond ambaye alijaliwa naye watoto wawili, wa kiume na kike hivyo anaaminika kumjua vizuri staa huyo wa Wimbo wa Tetema kuliko wanawake wengine kadhaa aliowahi kutoka nao. Kwa mujibu wa Zari, hizo ni dalili za mpasuko kwenye penzi lao.


Ni Lynn ndiye aliyeibua gumzo hivi karibuni baada ya kuachia picha zilizomuonesha akiwa kwenye kitanda ambacho Tanasha naye aliwahi kuachia picha akiwa kwenye kitanda hichohicho.


TANASHA AMTETEA


Katika kumtetea Diamond, Tanasha aliandika kwenye ukurasa wake wa Snapchat; “Hicho ni kitanda kutoka Danube. Kila mtu anaweza kuwa nacho.”


USHAURI KAMA MOBETO


Zari ambaye umri umekwenda kuliko wote, yaani Tanasha, Diamond na Lynn alimpa Tanasha ushauri huo wa kuwa makini kama alivyowahi kufanya kwa mwanamitindo Hamisa alipokuwa na Diamond kabla ya kuzaa naye mtoto mmoja na penzi lao kuota mbawa.


“Wakati mwingine, jambo zuri unaloweza kufanya ni kufunga mdomo wako na kuacha macho yako wazi ili yaone. Ukweli huja mwishoni mwa jambo lolote,” aliandika Zari kwenye ukurasa wake wa Snapchat, ujumbe ambao ulielezwa kumlenga Tanasha. Ushauri wa Zari kwa Tanasha umekuja wakati ambao mpenzi huyo wa Mondi amekuwa akipotezea tetesi za jamaa yake huyo kurejesha majeshi kwa Lynn.


TANASHA AFUNGUKA


Katika moja ya chati zake kwenye Snapchat, Tanasha aliandika; “Sasa ishu ni hii, kwa kawaida huwa sipendi kuwapa watu ‘attention’ wanayoitaka kwa njia ambayo siyo sahihi, lakini nikichokozwa kwa kiasi hiki ambapo jina langu linachafuliwa, huwa siwezi kujizuia.


“Kwa hiyo kama wengi mlivyosikia tetesi zinazosambaa (kuwa Diamond alikuwa chumbani na Lynn), wengi wenu mnaamini ni kweli. Siwalaumu ninyi kwa sababu tetesi hutengenezwa na watu wenye chuki.” Ndoa ya Diamond na Tanasha imekuwa ikisubiriwa kwa hamu tangu ilipoahirishwa Februari 14, mwaka huu ambapo imekuwa haijulikani itafungwa lini.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages