NAOMBENI USHAURI:BOYFRIEND WANGU ANATAKA NIMPE RAHA NA UTAMU WAKATI MIE BADO BIKIRA,NIFANYEJE? - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 15, 2019

NAOMBENI USHAURI:BOYFRIEND WANGU ANATAKA NIMPE RAHA NA UTAMU WAKATI MIE BADO BIKIRA,NIFANYEJE?




Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23,naishi kigamboni,nimemaliza chuo mwaka jana.Nina Tatizo linanisumbua,nashukuru Mungu nimeweza kuvumilia kwa muda mrefu bila kulala na Mwanaume.Nimeweza kuhifadhi zawadi nzuri yenye thamani kubwa ambayo kwa mwanamke mwenye Heshima zake anastahili awe nayo kwa ajili ya kumpa mume wake baada ya kufunga Ndoa(namaanisha kuwa mie bado bikra). 
Tatizo Linalonisumbua ni kwamba kila muda Boyfriend wangu ananisumbua anataka nifanye nae mapenzi,nikimnyima anasema kuwa simpendi,na kiukweli mi nampenda tena sana,na ninajisikia vibaya ninapomuona mpenzi wangu amenuna amekosa furaha,Kwani hakuna Njia nyingine ya kumfanya aniamini kuwa nampenda bila kufanya nae mapenzi? Ninachotaka mimi Nimpe Penzi kwenye Usiku wa Fungate kama Zawadi Special kwa ajili yake lakini Naogopa nikiendelea kumnyima nahisi ataniacha au atanisaliti akapate ninachomnyima kwa wanawake wengine,Naombeni Ushauri Nifanyeje?


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages