Haina maana kuwa ukijihami kuwa tayari una mtu ndio itasaidia wewe kumpata mtu sahihi na mwenye mapenzi ya kweli, ila huenda ikawa njia rahisi zaidi ya kumpata mtu tapeli,
kicheche na mdanganyifu wa mapenzi. Ambaye atakusababisha maumivu makali mwishoe uanze kusema wanaume wote hawafai kabisa.
Kwa sababu kama ulishaanza kwa kumwambia kuwa una mtu wako ila bado akalazimisha akutake na akakupata unaelewa nini hapo? ....
Kumbuka kwamba, siku zote mwanaume mstaarabu huheshimu ndoa au mahusiano ya watu. Hivyo ukimwambia kuwa tayari upo na mtu wako busara atakayoifanya ataachana na wewe kukufuatilia, ila mwanaume muhuni hatoacha kukufuata wala hatojali. Maana kwake kuingililia ndoa au mahusiano ya watu kwake ni jambo la kawaida na wala hajali.
Nakushauri kabisa...
Kama kweli huna mtu ni bora uwe muwazi tu, usimfundishe mtu uongo na utapeli mtu anayekuhitaji. Maana akishafanikiwa kwako hatoishia hapo ataendelea kutongoza wake za watu bila uoga na kujali.... Zingatia hili..
No comments:
Post a Comment