Daktari awaonya wanawake na wanaume kunyoa sehemu za siri - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 11, 2019

Daktari awaonya wanawake na wanaume kunyoa sehemu za siri



Daktari wa wanawake ameonya dhidi ya kunyoa sehemu za siri eti kama njia moja kudumisha usafi

Kulingana na Dkt Ignitius Kibe, Mungu aliumba binadumu awe na nywele hizo anapobalehe kwa sababu kadhaa na pia zina umuhimu sana hasa wakati wapenzi waposhiriki kitendo cha ndoa.

Akiwa kwenye mahojiano na runinga ya Citizen Jumatano Machi 27, daktari huyo alisema nywele hizo husaidia sana wakati wa kitendo cha ndoa.

Aidha, daktari huyo alisema sio salama kuzinyoa kwani mtu anaweza pata vipele na michubuko kwenye sehemu za siri

" Mimi kwangu binafsi napendelea hizo nywele ziwepo, zina umuhimu sana wakati wapenzi wanaposhiriki kitendo cha ndoa," Dkt Kibe alisema.

Daktari huyo alisema wale ambao hunyoa nywele hizo wanahatarisha maisha yao kwani ni rahisi kuambukiwa magonjwa ya zinaa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages