Wizara ya Utalii nchini Uganda imewaainisha wanawake wenye umbile, makalio makubwa na miguu minene kuwa ni kivutio cha utalii nchini humo.
Akizindua shindano la "Miss Curvy" ambalo litaonyesha shepu halisi ya wanawake wa Kiafrika ambalo litawawezesha wanaweke kuonyesha makalio yao makubwa, kiongozi huyo amesema Uganda ina wanawake warembo wenye shepu za kuvutia na hivyo serikali itawatumikia wanawake hao kukuza sekta ya utalii.
"Tuko na wanawake warembo sana humu nchini, wenye shepu ya kudondosha mate kwa kila mwanaume, mbona tusiwatumie hawa watu kukuza sekta ya utalii humu nchini?", amesema Waziri Kiwanda.
Ann Mungoma ambaye ni mwandalinzi wa shindano hilo amesema, sekta ya utalii itaboreshwa punde tu mwanamke mwenye umbo na makalio ya kuvutia atakapochaguliwa, na kudai kuwa Waafrika wanapaswa kuelewa kuwa watu wanene pia wanaweza kuwa warembo wala sio wembamba pekee.
No comments:
Post a Comment