Nimevunja uchumba rasmi,sitaki tena kuoa! - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 9, 2019

Nimevunja uchumba rasmi,sitaki tena kuoa!



Mimi ni kijana umri wangu ni miaka 32,ni msomaji mzuri wa jukwaa hili,japo sio mchangiaji sana!

Nimeamua kuja na ID mpya ili kujieleza kwa uhuru zaidi!
Nimekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 3 sasa,na tulikubaliana na mpenzi wangu kwamba mwezi February, nipeleke mahari,(I was very comfortable)

Kilichotokea jana,kimenifanya nikate tamaa kabisa ya kufikiria kuoa,labda nipate muda wa kupumzika sana,na sijui nipate mwanamke wa namna gani!!?

To make a story short,ni kwamba Jana tulikubaliana kufanya tathmini ya uelekeo wa uchumba wetu,tulitoka na kwenda mahali tulivu nje kidogo ya jiji,tulifanya hivyo tukiwa na amani tele!

Ilipofika majira ya saa kumi hivi nikaona kama anakosa utulivu,kila mara anashika simu na kuonekana very busy charting, nikamwambia we have to concentrate on what brought us here na sio unakuwa busy na simu kiasi hicho!

Alionekana kunielewa lakini kwa jicho la kisaikolojia niliona bado hayupo normal,nikaamua kuchukua simu zote na kuziweka mezani,karibu na mimi,akakosa amani kabisa!!!
Mara ikaingia sms, "Baby sasa mbona haujanitumia ile pesa" (niliisoma kupitia WhatsApp notification),baada ya kuona hiyo msg moyo ulinilipuka,nikaamua kufingua SMS hiyo ili nijue kinachoendelea!

Nilipofungua SMS nikabaini kwamba anatiwa na dereva boda boda,kilichoniuma zaidi ni kwamba natafuta pesa kwa jasho sana,ili kuiandaa kesho yetu,yeye anatoa pesa kumpa huyo boda boda,haki ya Mungu maumivu niliyopata hayaelezeki!

Mchumba wangu amefikia hatua ya kufanywa kinyume na maumbile,nimeshangazwa kwa viwango vya juu sana,nilijitahidi sana kujizuia ili nijiridhishe kikamilifu juu ya mahusiano yao!

Nilikuwa mpole machoni,lakini niliyekasirika sana moyoni,nikamtaka aniambie ukweli,ili ikiwezekana nimsamehe!

La haula!!!ananiambia ni kweli amekuwa naye kwenye mahusiano kwa mwaka sasa,na jamaa ndo amemfundisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile,halafu anaomba nimsamehe!!!

Nilipoyasikia maneno hayo mwili mzima ulipigwa ganzi,hasira zilikuwa na nguvu kuliko uwezo wangu wa kuzidhibiti!
Ilinilazimu kuondoka mazingira kwa haraka sana ili kuepusha madhara ambayo yawezekana ningeyafanya!

Leo amenipigia simu,sikupokea,ameniandikia ujumbe kwamba haoni tena sababu yakuishi,bora afe,nimemjibu kwa kifupi tu,kwamba "kufa"

Baada ya hapo,nikaa na kutafakari sana,kwamba kama ningekuwa na wapenzi angalau watatu,hata nisingepata maumivu makali kiasi hiki,na pengine ningeanza mchakato na mwanamke mwingine,sasa uaminifu wangu unaniponza!!!

Nakutakia kila la heri M.
NITAANZA TU UPYA!MUNGU MKUBWA NITAMPATA ATAKAYENIHESHIMU KABLA NA BAADA YA NDOA!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages