Ndugu zangu, naombeni nisieleke vibaya.. Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26. Nina mwaka wa kwanza tangu nianze kujitegemea mara baada ya kumaliza shule. Nimepanga kwenye nyumba moja iliyoko maeneo ya Mbezi.
Tatizo langu ni kwamba nimetokea kumpenda sana baba mwenye nyumba wangu ambaye ana watoto na familia. Kila nikijibaraguza siwezi.
Nimefanya kila mbinu kuzificha hisia zangu lakini nimeshindwa.Kimsingi simpendi mwanamume mwingine zaidi yake.
Nisaidie kuniepusha na mtihani huu mgumu.Asanteni
Anna
No comments:
Post a Comment