Wakuu habari za wakati huu.
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wanaume kwamba wadada wa siku hizi hawana mapenzi ya dhati; wanaangalia zaidi pochi.
Hili lina ukweli kwa kiasi fulani....lakini kuna type ya wanaume ambao kifupi niseme tuu kwamba hawajitambui.
Waweza kuona mtu ana miaka 25, direction ya maisha yake haionekani kabisa....bado anaishi nyumbani kwa wazazi au kwa mjomba..yani hajawa na uwezo hata wa kupanga chumba chake cha elfu 30 na wakati huohuo hasomi wala nini..yani yupo yupo tu na anategemea akioa awe kichwa cha nyumba eti.. Anachojua yeye ni 'I love u baby' kila baada ya nusu saa.
Hivi mpaka kufikia umri huo mtu hana mawazo ya kutengeneza future huko mbeleni itatengenezeka kweli?
Mwanamke atampenda mwanaume na umaskini wake iwapo mhusika mwenyewe anaonesha dalili za kujikwamua....kama future yako haionekani japo kwa tochi mwanamke anayejitambua atakukimbia tu na utabaki kulalamika watu hawana mapenzi ya dhati....hakuna mtu anayependa mizigo bwana..
Samahani kama imekugusa...
No comments:
Post a Comment