Kwa aina ya uchawi aliofanyiwa jirani yangu kwa kutembea na mke wa mtu nang'atuka rasmi ili nami yasije kunikuta! - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 27, 2019

Kwa aina ya uchawi aliofanyiwa jirani yangu kwa kutembea na mke wa mtu nang'atuka rasmi ili nami yasije kunikuta!



Asikuambie Mtu bhana kama kuna Watu wanajua ' Kuroga ' basi ni Watanzania na hasa hasa ukitaka kujua aina mpya na mbalimbali za ' Kurogwa ' jifanye unakosea, tongoza Mke wa Mtu halafu mwenyewe akijua subiria ' Kifuatacho ' Kwako.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Jirani yangu mmoja sasa ni Siku ya Kenda / Tisa hanyi kabisa ( hatoi Haja Kubwa ) lakini muda wote akikaa anasikia hamu ya Haja inakuja ( Makimba yanaonyesha Ushirikiano ) lakini akienda tu Uani / Msalani akijikunja ili ayateremshe yanakoenda hayatoki kabisa.

Kama hiyo haitoshi akisema tu atoke Uani / Maliwatoni na kuja Kukaa Sebuleni ile hali ya Kusikia Haja inakuja na huwa inapungua tu pale ambapo akishika Kopo la Chooni ambapo kwa hali ilivyo sasa hata kama ukisema uende Kumtembelea Nyumbani Kwani lazima tu utamkuta ameshika Kopo la Chooni na kama asipolishika tu basi ile hamu ya Haja Kubwa huja tena kwa Kasi zote kama Mafuriko ya Dar es Salaam.

Kama Rafiki yake ilibidi niombe Mazungumzo nae ili niweze kujua tatizo ni nini na kwakuwa tunaheshiana sana Jirani yangu mwenyewe kwa Kinywa chake amesema kwamba kumbe Mume wa Mwanamke ambaye mara kwa mara alikuwa na Mahusiano nae Siku kama 13 zilizopita alimuonya aachane na Mkewe na kwamba akiendelea ' Kumtafunia ' kitakachomkuta basi asije Kulaumiwa.

Hivi kama Mtu anaweza kuwa na uwezo wa ' Kumroga ' hivi Binadamu mwenzie kisa tu anatembea na Mkewe hivi Siku kwa mfano nae akija kusikia GENTAMYCINE ' anambandulia ' huyu Mtu si anaweza hata akaihamisha Sura yangu nzima na akaiweka ' Ugokoni ' mwangu na Visigino vyangu akavihamishia mashavuni?

Leo natangaza rasmi ' Kung'atuka ' huu utaratibu wa Kupenda Kutembea na Wake za Watu na niwaombe pia na Wanaume wenzangu wenye hii tabia kuwa jamani acheni kwani kuna Raia / Njemba zinajua mno ' Kuroga ' na ' wanaroga ' vibaya mno. Na kama muda huu hapo ulipo upo na Mke wa Mtu na bado hujaanza ' Kumbandua ' tafadhali mwambie tu avae na amuwahi Mumewe kabla nawe hayajakukuta ya huyu Jirani yangu.

Nawasilisha.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages