SABABU 4 ZA KUOA/KUOLEWA NA KUISHI MAISHA YA FURAHA BAADA YA NDOA - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 6, 2019

SABABU 4 ZA KUOA/KUOLEWA NA KUISHI MAISHA YA FURAHA BAADA YA NDOA










Kama upo katika uhusiano wa muda mrefu kwa sasa na unajiuliza kwamba kweli unaweza kuuvaa huu wajibu mpya wa kuishi na mtu maisha yako yote kwa kitu kinachoitwa ndoa, zifuatazo ni sababu 4 za kuingia katika ndoa ambazo unapaswa uzizingatie. Kama utazitafakari kwa makini hizi sababu, utaelewa upande mzuri wa ndoa na utajua kama upo tayari au la!.
#1 Ni ahadi kubwa sana. Hakuna uthibitisho mkubwa wa upendo kama kumuuliza mpenzi wako kama mnataka muoane. Usiiangalie ndoa kama vile kofuli lisilokuwa na ufunguo. Ione ndoa kama mojawapo ya njia unayoweza kuweka ahadi yako kubwa kwa mpenzi wako kama ishara ya upendo
#2 Una share maisha yako na mwingine. Sisi kama binadamu tumeumbwa kama kiumbe ambacho tunaweza kuingiliana na kushirikiana kwa pamoja katika jamii. Kuishi maisha ya peke yako inaweza ikaonekana kuwa nzuri kwa mwanzoni, lakini inafika wakati, kila mmoja wetu anajisikia kuhitaji mtu mwingine atakayekua anamuangalia, na kuwa na mtu mwingine ambaye unaweza ku shea nae furaha na matukio ya huzuni pia.
#3 Umesha enjoy sana maisha ya kuwa peke yako. Unakumbuka kipindi una miaka ya ujana na kipindi wewe upo single ulivyokua? Na sasa umebadilika, na hii itakuonesha kuwa maisha yamebadilika na umekuwa mtu wa tofauti, na unahitaji kuwa na mtu wa kushirikiana nae maishani, na si tu wakulala nae usiku.
#4 Hatua za maisha. Kama nilivyosema hapo awali, maisha ni mchezo wa hatua. Na kama umejiandaa kiakili na kimwili na kisaikolojia kuingia hatua nyingine, mawazo yako na akili yako yatakushawishi kuingia katika hatua hiyo inayofuata kwa kukuonesha faida zake. Na ndoa ni hatua muhimu sana katika maisha. Kama kweli unampenda mtu, jitwike hilijukumu. Utajipatia uzoefu mpya wa maisha ambao haukuuzoea na inaweza kukusaidia kuendeleza maisha




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages