ISHARA 5 KUONYESHA MWANAMKE ULIYENAYE ANAKUTUMIA HALAFU AKUTENDE - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 11, 2019

ISHARA 5 KUONYESHA MWANAMKE ULIYENAYE ANAKUTUMIA HALAFU AKUTENDE

Wazungu hupenda kusema ‘Love is blind’, yaani mapenzi ni kipofu. Usemi huu ni wa kweli kwa sababu unaweza kuona wapenzi wawili wamependana kiasi cha kuwa hata ukimkanya mmoja wao kuhusiana na jambo flani hawatakuelewa.
Ni vizuri kuwa katika uhusiano wa kimapenzi aina hii. Hukuza upendo. Lakini swali linakuja pale ambapo unajiuliza iwapo huyu unayempenda naye anakupenda?
Wanaume wengi wanashindwa kutambua kati ya kupenda na kutendwa. Wengine wanazama katika mapenzi bila kuyaelewa na mwishowe utaskia katika runinga na maredioni kuwa mwanaume amejinyonga kisa ni mwanamke ama utaskia mwanaume amemuua mpenzi wake kisa kamcheat.
Well, kabla mambo yafikie hapo, lazima ujue iwapo huyu unayempenda anakuchezea ama yuko serious nawe. Ndio maana leo hapa kitovu cha mapenzi tumekuja na ishara ambazo unaweza kuzitambua iwapo mwanamke unayemchumbia yuko serious ama yuko tu na wewe kukutumia halafu akishamaliza tu akuteme kama mate.
Ishara #1. Unajihisi hujakamilika.
Ukiwa na yeye unajihisi kuwa kuna kitu ambacho kinakosekana. Hii mara nyingi inatokea kwa sababu hamgawi hisia moja. Hii ndio inakufanya uhisi kuna kitu kinachokosekana. Unajaribu kila uwezavyo kumfanya akupende zaidi lakini kila mara ukijaribu unafeli na unauangukia mtego wako mwenyewe.
Ishara #2. Yeye ndie anayemiliki uwanja.
Unahisi kuwa ni wewe pekee unayejitolea kufanya kila kitu. Unajifua kila wakati ili uhakikishe unampendeza lakini kwa upande wake hakuna kitu chochote ambacho anajitahidi kukuridhisha nacho.
Kama yeye ndie anamiliki uhusiano wenu haimaanishi kuwa anakutumia lakini anajaribu kukuonyesha uhusiano wenu si wa afya. Uhusiano mwema ni ule ambao unahusisha watu wawili nyakati zote.
Ishara #3. Wewe ndio nguzo yake.
Kama anahitaji sapoti kihisia, wewe ndie anakukimbilia. Mazungumzo yake mara nyingi huzunguka maisha yake na shida zake ambazo anazipitia. Lakini je unapopatika na shida? Anakusikiliza ama anakupuuza? Well, kama hana time na wewe kuskiza shida zako basi hayo si mahusiano ya kudumu.
Ishara #4. Anakutuza wakati umemfanyia jambo zuri kwake.
Hapa ni kama tu vile ambavyo unamwekea farasi nyasi mbele yake ili awe na motisha wa kuendelea kukimbia. Kiufupi anakutumia vibaya ili ufanye kitu ama jambo ambalo ulikuwa hutaki kufanya lakini mwisho wa kumfanyia jambo hilo anakupa hizo nyasi kama zawadi. Nyasi hapa inaweza kuwa ni kukupa uroda, kujipa majukumu ama mapenzi ya muda. Mambo kama haya hayahisabiki kama upendo ama uhusiano kabisa.
Ishara #5. Ni mtu asiyeeleweka.
Ule wakati ambao umechoshwa na tabia zake mbaya unamwona anajileta chini kabisa. Ananyenyekea mbele yako huku mikono yake yote anaikumbatia kwako. Imefikia ule wakati ambao yuko karibu kupoteza kila kitu so analeta visababu ambavyo havieleweki kabisa.
Mfano mchunguze kama anafanya jambo kama hili. Je huwa anakuwa mnyeyekevu ama kulia wakati ambao unajaribu kumlazimisha akupatie nafasi uwe pekeako, yaani umechoshwa naye so unataka akuachilie uyafikirie maisha yako? Well, hapa hudeal na mwanamke ambaye haeleweki bali unadeal na mwanamke ambaye anakutumia.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages