Suala la mwanaume kuwa na mpango wa kando au nyumba ndogo sio geni kabisa lakini miaka mingi iliyopita mwanamke huyo amekuwa hazungumziwi kabisa na wanandoa kama mwanamke unakuwa unamjua mwanamke anayekuchukulia mumeo lakini huwezi kufanya lolote.
Kwa miaka ya nyuma nyumba ndogo ilikuwa inatumika pale mwanaume anapokuwa haridhishwi na mke wake hivyo hutafuta nyumba ndogo na ilikuwa aibu kubwa kwa mwanaume kuwa nayo lakini tukubali tukatae mambo yamebadilika dunia ya sasa hata jina la nyumba ndogo limebadilika sahivi ni mchepuko wanajulikana hivyo hata mwanaume haoni aibu kuwaambia washkaji zake juu ya mchepuko wake.
Hata kwa wanawake mambo yamebadilika hawaoni soo kuwa mchepuko wa mwanaume anaona akiwa na mke wake atafaidika kutunzwa lakini pia atakuwa na nafasi ya kuwapanga wanaume wengine bila kuchungwa na yule mwanaume wake kwani tayari ana familia yake na mke.
Lakini nini kitatokea kama unataka kuwa zaidi ya mchepuko? Unataka kuwa mke wa mtu fulani Hizi ni mbinu kadhaa za kumteka mwanaume huyo;
1. Jiweke tofauti na mwanamke wake
Mwanaume yoyote ukiona anaenda kutafuta mchepuko basi jua wazi mahusiano yake na mwanamke wake kuna dosari fulani hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi na kujua nini anakosa na nini hapendi kwa mwanamke wake ili wewe ufanye tofauti na uwezo kumteka.
2. Jitahidi kuwa smart ukiwa naye
u-smart tunaouongelea hapa ni usmart wa akili kichwani na usmart wa kimavazi ni muhimu kwani kwanza hakuna mwanaume anayetaka kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye hana akili za kimaisha lakini pia kuwa msafi wa kimavazi ni muhimu kwani mwanaume na mwanamke wanapokaa kwenye Mahusiano kwa miaka mingi huzoeana na kusahau kuna kitu kupendeza kwa ajili yake kwaiyo wewe sasa ndio muda wa kuchunguza ujue anavutiwa na mavazi gani na wewe uyatinge.
No comments:
Post a Comment