KUWA MNYENYEKEVU KWENYE NDOA/MAHUSIANO SIO UPUMBAVU - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2019

KUWA MNYENYEKEVU KWENYE NDOA/MAHUSIANO SIO UPUMBAVU









Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu,,hata ungekuwa umemkosea nini,ukijishusha,ukanyenyekea analainika,,labda awe na mapepo ndo unyenyekevu wako hautagusa moyo wake,,mume hafokewi,mume hagombezwi,,mume hafanyiwi jeuri na kiburi,,akinuna na wewe unanuna,asipokutafuta na wewe humtafuti,,utapoteza ndoa yako,, 
Ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba,,asipokutafuta mtafute,asipo ongea na wewe,wewe ongea nae,,hakunaga mke anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe,,kunyenyekea hakukugeuzi housegirl na kupoteza nafasi yako kama mke,,ila kiburi na jeuri ndo vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana,,ujeuri weka pembeni, ndivyo walivyofanya waliodumu kwenye ndoa zao,,kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages