SOMA HAPA MAANA YA MSAMAHA NA FAIDA ZAKE - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 10, 2019

SOMA HAPA MAANA YA MSAMAHA NA FAIDA ZAKE





*Msamaha ni nini?*

-Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe.

- Msamaha ni kitendo cha kurudisha uhusiano wa awali uliovunjika.  Kusamehe ni kumfutia mtu hatia.

*Zifuatazo ni faida za kusamehe:-*

*1.Tunasamehe kwasababu kusamehe ni tabia ya Mungu* Tunapaswa kusameheana kwani muasisi wa msamaha ni *Mungu mwenyewe* na kama Mungu angehesabu maovu yetu nani angesimama?


*2.Tunasamehe ili tuweze kusamehewa.*
Unapaswa kusamehe kwa faida yako mwenyewe siyo kwa faida ya mkosaji na  wewe hebu *mwachie Mungu apambane na watesi wako wala usilipe kisasi.*

*3.Unasamehe ili uwe na amani.* Unaposamehe unakuwa unapata amani ya moyo. Mtu ambaye anavumilia uchungu ulioumbika ndani ya moyo na hataki kuachilia fundo hilo lazima litamtesa na atakosa amani ya moyo. Atahangaika na huku uchungu ulioumbika ndani ya moyo ukiendelea kumtafuta.

*4.Unasamehe ili uwe na furaha.* Kwa kweli ukiangalia watu wanaokataa kusameheana huwa hawana furaha kabisa katika mioyo yao. Kama unaishi katika mahusiano yoyote na mara nyingi huwa watu si wakamilifu basi msamaha ndio kiunganishi chenu ambao utarudisha uhusiano uliopotea

*5.Tunasamhe ili tuwe na afya njema*
 Uponyaji wa kweli unaanzia moyoni. Kama mtu anasamehe kutoka moyoni basi huo ni msamaha wa kweli na ni msamaha unaoongozwa na  *huruma ya Mungu ndani yake.* Watu hawataki kusamehe ndio maana wengine afya zao ni dhaifu. Uchungu ulioumbika ndani ya moyo unaendelaa kuwatafuna.
*Usizeeke kabla ya wakati kwa ajili ya kutosamehe watu wengine*


HASARA ZA KUTOKUSAMEHE

6.Kutosawasamehe watu kunakufanya ujikinai wewe mwenyewe.*
Unajiona wewe ni mtu ambaye hustahili kuwepo hapa duniani. Utajiona wewe hauna maana hapa duniani utakua unakaa peke yako peke yako.
Huna furaha, amani, upendo. Maisha yako yanakuwa yamejaa sumu na majeraha moyoni ugonjwa umekuwa mkubwa na wewe hutaki kuupatia dawa ya kuuponya na dawa yake ni msamaha tu.

*7.Kutokusamhe kunaongeza maadui katika maisha yako.*

Jaribu kuangalia katika maisha yako Yule anayesamehe na asiyesamehe nani anakuwa anaongeza maadui?

 Utaongeza maadui na utavunja uhusiano na watu hivyo utakua unaishi maisha ya umimi.

*Maisha ya binadamu ni maisha yenye uhusiano kama husamehi basi unajitengenezea duniani yako mwenyewe.*

*8.Kutosamhe kunaleta mapasuko wa kifamilia.*

Katika hali ya kawaida jaribu kuangalia katika jamii yako ni familia ngapi zimesambaratika kwasababu ya kutosameheana ?

 Kusamehe ni faida kwa kila familia bora inayotaka amani na furaha, mipasuko katika familia itaendela kuwepo kama watu wasiposameheana.

*9.Kutosamehe kunaleta unyonge wa moyo yaani huzuni.*

 Ukiwaangalia watu wengine unawaonea huruma wanaishi maisha ya huzuni wakati
*falsafa ya maisha ni furaha hapa duniani.*
Tunatafuta kila siku ili tuweze kuwa na furaha. Inuka leo na nenda
*kazike hilo jeneza la huzuni na kuwa huru na maisha yako.*
*Huoni ni utumwa kuwabeba watu moyoni?*

*10.Kutosamehe kunawafanya watu kukimbia makazi na ofisi zao.*

 Kwa mfano, watu waliokoseana na hawataki kusamehana huwa wanaishi maisha kama ya paka na panya. Akimuona mwenzake huyo anakuja anakimbia kama yuko nyumbani anakimbia, kama ni njia anabadilisha kabisa ili wasionane na kusalimiana. Unakuta watu wengine wanakimbia kabisa ofisi zao kwasababu ya kutotaka kusameheana. Kwanini uendelea kuishi Maisha Haya ?

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages