Sababu 4 za mwanamke kutopenda kuanzisha tendo la ndoa faragha - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 6, 2019

Sababu 4 za mwanamke kutopenda kuanzisha tendo la ndoa faragha

SOMA ZAIDI MAMBO YA MAPENZI NA MAHUSIANO KUPITIA HAPA

Wanaume huonekana kushangazwa sana na tabia ya wanawake kutopenda kuanzisha tendo la ndoa wanapokuwa faragha. Licha ya wanaume kutokuwa na tatizo la kuanzishatendo la ndoa faragha, wakati mwingine wanaume hutamani kuona wanawake wakifanya hivyo pia.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazowazuia wanawake kuanzisha tendo landoa wanapokuwa faragha na wapenzi wao;-
  1. Hofu ya kukataliwa.
Wanawake wengi huogopa kuanzisha tendo la ndoa kwa hofu ya kukataliwa. Wanaumia sana wanapoanzisha tendo la ndoa na wanaume hawaonyeshi ushirikiano wa kutosha, hivyo wanawake wengi hupendelea kuwaachia wanaume usukani huo kwa hofu ya kukataliwa.
Ili kumsaidia mkeo kuondokana na hofu hii ni vyema kuonyesha ushirikiano pindi anapo ashiria uhitaji wa tendo la ndoa. Muongezee ujasiri kwa kumweleza jinsi unavyopenda anapokuwa kiongozi pindi mnapokuwa faragha. Jitahidi kuujari uhitaji wake hata kama uko bizze
2.Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Usikose Hii: Maumivu Unapofanya Tendo La Ndoa (Dyspareunia)
Mwanamke hatojisumbua kuanzisha chochoteikiwa kama anapata maumivu wakati wa tendo la ndoa. Kama tendo la ndoa linamletea maumivu, hawezi kufurahia tendon a kama hafurahii usitarajie mkeo kuanzisha jambo asilolifurahia hususani tendo la ndoa.
Wakati mwingine wanaume wengi hukimbilia kufanya tendo la ndoa pasipokuwa na maandalizi ya kutosha, matokeo yakekupelekea mwanamke kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa. Vilevile inawezekana maumivu hayo yanasababishwa na magonjwa ya zinaa (Sexual Transmitted Diseases), hivyo ni vyema kufanya utaratibu wa kupata huduma za kiafya mapema katika hali kama hii
3. Baadhi ya wanawake huchukulia kitendo hicho kama desturi.
Kwa baadhi ya wanawake huamini kuwa wanaume ndio wanaopaswa kuanzisha mambo kitandani. Huamini kuwa endapo kama watakuwa waanzilishi wa tendo la ndoa ni rahisi kuonekana Malaya mbele za waume zao. Hivyo ili kuepukana na tatizo hili wanawake wameamua kutojichukulia madaraka ya kuwa waanzilishi wa tendo la ndoa.
Jambo la msingi hapa ni kwamba mwanaume anapaswa kumfanya mkewe ajisikie kuwa huna tatizo na yeye kuwa mwanzilishi wa tendo la ndoa pindi mnapokuwa faragha. Mwache naye atambue ya kuwa unatamani kumuona wakati mwingine yeye akiwa mwanzilishi wa tendo. Uvumilivu unahitajika katika hili
4. Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Usikose Hii: Tendo la Ndoa: Mkeo Anakosa Hamu Ya Tendo La Ndoa? Msaidie Hivi
Usitarajie mkeo kuanzisha tendo la ndoa ikiwa kama anakosa hamu ya tendo mara kwa mara. Wakati mwingine kutokana na msongo wa maeazo yanayosababishwa na kazi nyingi, wanawake wengi wamepoteza hamu ya tendo la ndoa.
Msaidie kuondoa msongo wa mawazo kwa kumfanyia massage na kumwandalia ziara ya siri ya kimahaba. Yawezekana ndicho anachotaka na na kinachoweza kumsaidia apate hamu ya kufanya tendo la ndoa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages