Ushawahi kuwa na mahusiano na mwanamke halafu mara akapoteza hisia na wewe? Anaonekana siku moja anajiskia na wewe mara ghafla anakwambia amechoshwa na wewe? Unatumia mbinu zako zote za maujanja kumfanya arudishe maslahi kwako lakini ni kama kupigia mbuzi gita. Mwishowe anakataa kujibu ama kupokea simu zako. Ama anakutumia jumbe ya:
"Kuanzia leo naona heri tuwe marafiki tu"
So tatizo hapa nimekujaje?
Well, tatizo ni kuwa utakuwa umelileta wewe mwenyewe. Kujaribu kutopatikana na majanga kama haya tena, nimeamua kuorodhesha makosa makubwa wanaume hufanya kwa mwanamke.
1. Kujaribu kumpendeza
Kama unashangaa inawezekanaje kumpendeza mwanamke ikawa kosa kubwa la kumfanyia mwanamke basi ni dhahiri ya kuwa wewe ushawahi kufanya kosa kama hili. So makosa makuu ya kumpendeza mwanamke ni nini? Mara nyingi huletwa na sababu mbili kuu:
Kuzungumza sana kujihusu- wanaume wengine wakiwa wanaongea na mwanamke kazi yao sana ni kujieleza kuhusu maisha yao, matukio waliyoyafanya nk bila ya kumpa mwenzake nafasi ya kujieleza. Hebu chukulia unazungumza na mtu ambaye anaongea yeye pekeake bila kukupa nafasi ya kumjibu.
Kujisifu na mali ulionayo- kosa jingine ni kuwa na tabia ya kujisifu kuhusu vitu unavyomiliki. Ingawa wewe utaona ni sifa, kwa mwanamke huwa ni tofauti kabisa.
2. Kukubaliana na kila kitu atakachosema
Mwanaume ambaye hana uwezo wa kukataa chochote kutoka kwa mwanamke basi ni ishara ya kuwa baada ya muda mfupi wa mahusiano wataachana.
Kulingana na saikolojia ya wanawake, wao hupenda kuongozwa na wala si kuongoza. Hivyo wakiona ya kuwa kila kitu atakachosema mwanaume anakubaliana bila kupinga basi kwa kawaida huona ya kuwa unataka yeye ndiye aendeleze mahusiano yenu. Pia mara nyingi huona kama kuwa na wewe kimahusiano kunaboa.
Hapa nataka ufahamu ya kwamba sijasema lazima upinge kila kitu mwanamke anachosema wala sijasema uanze vita na mwanamke ili kukabiana na changamoto ya kutemwa. La. Mwanamke kawaida anapenda vioja katika maisha yake. Leo ukiwa na tabia hii, kesho mjeuzie tabia nyingine. Huku kutayafanya maisha yenu yawe ya kuvutia kila wakati.
3. Kuitikia mahitaji yake kila wakati
Je wewe ni yule mwanaume ambaye akipigiwa simu na mpenzi wake anaacha shughuli zake zote ili kumjibu? Ama wewe ni aina ya mwanaume ambaye kila mahali mpenzi wako atakapoenda unakuwa kando yake?
Labda unaona kufanya hivi unatimiza tabia za kuwa kama gentleman, ama unajaribu kumridhisha mpenzi wako. Ikiwa hizi ni baadhi ya tabia unazofanya basi elewa ya kuwa hauko mbali kuachwa na mpenzi wako. Hii ni kwa sababu itafikia mahali flani mwanamke atakushusha hadhi kwa kuwa atakuona huna maisha. Ataona kwamba maisha yako yamezungukwa kwake.
Ni muhimu kwa mwanaume kuishi maisha yake yeye mwenyewe na wala si kuzungukwa na mwanamke. Hebu chukulia hivi, umemzoesha mwanamke kuwa kila mahali atakuwa akitembea na wewe, je ikifikia wakati wa kuchukua mkondo wa kuishi maisha yako kivyako itakuwaje?
4. Kumgharamikia anachotaka kupindukia
Kuna wanaume wengine wanafanya kosa la kujionyesha kuwa maisha yao ni ya juu kwa kumgharamikia mwanamke mahitaji yake yote anayotaka. Hii nikuanzia kumfanyia shopping, kumtoa deti sehemu za gharama nk. Labda ni kweli kifedha hauna tatizo lakini fahamu ya kuwa itafikia mahali fulani mwanamke ataanza kukushuku kama kweli wewe mapenzi yako ni ya dhati ama upo tu kumtumia halafu baada ya hapo unaachana naye.
Halafu pia ukimzoesha mwanamke kuwa kila wakati utakuwa ukimtolea fedha ikitokea kwa bahati mbaya ukose pesa basi mahusiano yenu yatakuwa na shida.
5. Unamgojea yeye aanze kuonyesha maslahi kwako
Huyu mwanamke unampenda lakini hutaki kumwambia kuwa umemzimia. Unamsoma akili na miondoko yake na umegundua kwamba pia yeye amekuzimia. Kwa hivyo unangojea nini?
Kosa ambalo wanaume wengine hufanya ni kuwa hawafunguki kwa mwanamke mpaka aone mwanamke anafunguka wa kwanza. Mwanaume kama huyu anacheza karata zake kwa kuangalia hatua gani mwanamke atachukua kama approach.
Kungojea mwanamke aonyeshe interest kwako ni kosa kubwa kwani mwanaume ndie ana majukumu ya kuhakikisha ya kuwa anamtongoza mwanamke na wala si mwanamke kumtongoza yeye.
So, wewe unatabia hizi ama ulikuwa na tabia hizi tulizozitaja? Mpira uko kwako sasa.
No comments:
Post a Comment