tunakutana wanajamvi wa Love katika kujifunza namna ya kukabiliana, kuzielewa na kuziishi changamoto mbalimbali tunazokutana nazo kwenye uhusiano, lengo likiwa ni kuboresha uhusiano huo na kuufanya uwe bora na wa kuigwa kwa mwaka huu wa 2019 na miaka mingine mingi tutakayojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Wanawake wengi wamekuwa wakiwalalamikia wapenzi wao kutokushinda nyumbani hasa siku za mapumziko, binafsi ninaamini kutokushinda huko kwa wanaume majumbani mwao kunachangiwa na vitu vingi sana ambavyo vinaweza kuwa ni vidogovidogo ila vyenye kukwaza.
Hakuna kitu kidogo, ila kizuri kinachopendwa na wapenzi wengi, hasa wa kike kama mpenzi, mchumba au mume wake kushinda nyumbani siku za mapumziko, wanawake wanapenda sana ‘kupetiwapetiwa,‘ wanapenda kupita mbele ya wenza wao wakijitingisha walivyojaliwa ili wenza wao waone. Wanapenda kupata muda wa kuzungumza na wenza wao kuhusu maendeleo ya familia yao japo kwa wiki mara moja na kuendelea.
Tatizo linaloonekana ni kwamba wanaume wengi huwa hawako tayari kubaki nyumbani kwa muda mrefu, siku ya/za mapumziko kwa kuhofia malumbano ya hapa na pale.
engine ni kwa sababu ya tabia za mwenza wake (wewe mwanamke), anaamini kwa jinsi ulivyo akisema ashinde tu ndani basi siku haiwezi kuisha bila kushikana shati au kutukanana, hivyo anaona bora kwenda zake kwa washkaji au baa kula masanga ili akirudi nyumbani muda wa migongoro na malumbano uwe angalau umepungua kidogo.
Ushauri wangu, angalia na rekebisha mapito yako, jiulize ni nini? Tabia ipi? kero au karaha zipi kwa mwenza wako zinazomfanya asishinde nyumbani au pengine ni tabia yako ya kidomodomo, gubu au kisirani?
Ukiweza kujua vyanzo vinavyomfanya mwenza wako asishinde nyumbani, itakuwa ni vizuri sana na kama utavifanyia kazi basi naamini mapenzi yako kwa mwaka 2016 yatakuwa matamu mno na yenye furaha.
Ingawa siyo wote wanakimbia kero za wenza wao, wanaume wengine ndiyo wanapopatia sababu ya kufanya mambo yao kama kula masanga, kukutana na marafiki, kufanya dili zao za nje ya ofisi na hata kuchepuka kwa wenye tabia hiyo.
Hebu fanya mwaka 2019 kuwa wa neema kwako, kama ni mwanamke jirekebishe, nawe mwanaume badilisha baadhi ya tabia zako, pengine ndizo chanzo kikubwa cha malumbano yenu yanayosababisha ninyi kukwidana, kutengana nakadhalika.
Kwa kuzingatia na kuufanyia kazi upungufu wenu ni hakika mtakuwa kama mnalipevusha upya penzi lenu, mwanamke badilisha vijitabia vyako vya ajabu, mwanaume pia fanya utaratibu wa kupumzika nyumbani siku ya mapumziko, watoto, mwenza wako wanakuhitaji, hata mifugo yako kama ng’ombe na mbwa nayo inakuhitaji ndiyo maana siku ukitaka kuipa chakula huwa inafurahi sana kwa sababu inahitaji uwepo wako
No comments:
Post a Comment