1. TAFAKARI CHANZO CHA TATIZO
una usemi kwamba ukitaka kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza ujue chanzo cha tatizo lenyewe. Ukishindwa kugundua chanzo cha tatizo, basi na wewe unakuwa sehemu ya tatizo.

2. MPE MUDA HASIRA ZIISHE
Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni wachache wanaoweza kuzidhibiti hasira zao. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga au kuharibu vitu akiwa na hasira.Baada ya kugombana, kila mmoja lazima atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi, ni kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira zipungue.

3. MPE NAFASI YA KUZUNGUMZA
Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na kumaliza kile alichokusudia kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua za kusaka suluhu, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku lililopo ndani ya moyo wake.
Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi mpaka dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa upole na sauti tulivu.

4. OMBA MSAMAHA
Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote na kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha. Neno ‘samahani’ ni dogo lakini lina maana kubwa kwa yule mtu anayelitoa na anayelipokea.
Hata kama unaona dhahiri kwamba kosa siyo lako, omba msamaha kwanza kisha baada ya hapo anza kumuelewesha mpenzi wako kwa upole. Lazima mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza kuepuka kuukuza ugomvi huo na kurudisha hisia za mapenzi.

No comments:
Post a Comment