Kuna bwana mmoja niliwahi kumskia akisema mwanamme kuwa na urafiki na mwanamke ni sawa na kutembea na muwa kama mkongojo ..hahaaa lazima utaula tu.
Asee hii kitu ni kweli kabisa,nakumbuka nikiwa chuo kikuu pale mlimani kuna binti tulitokea kuwa na urafiki,tena urafiki ule wanaousema kwa lugha ilokuja na majahazi ubest friend.Yule binti alitokea tu kuniamini kuliko hata marafiki zake wengine wa kike..alikua akiniambia habari zake karibia zote ,kuanzia mahusiano ,mambo ya familia yao hadi siri zake nyeti...na kiukweli aliniamini maana mimi nina haiba ya ukimya hivyo hakua na shaka ya kutapanyika kwa mambo yake .
Yule binti alikua na mtu wake wa muda mrefu aliekua amemaliza chuo tayari na mimi nilikua na msichana wangu pale pale chuo ambae walikua wanajuana vizuri na wanaitana wiii.Ilikuja kutokea huyu binti akaachana na mtu wake,tena kwa majonzi na huzuni kubwa...basi hapo nikajitahidi kuwa gentleman kama mzee Mengi nikawa namtuliza na kumpa maneno ya uhai kidogo.
Yule binti akaanza kurecover ile hali ila tatizo likaja akaanza kubadilika na kuanza kumchukia huyu demu wangu.Sikuelewa tatzo ila nikawa naona utofauti sio kama zamani...ila alikuja kunambia siku ambayo tuligegedana na kusema kuwa alikua akiona wivu sana juu ya mimi na yule binti.
Siku hio ndo nikakumbuka ile kauli ya muhenga ya muwa kuwa mkongojo.
Mkiwa na urafiki baina ya he na she lazima mmoja atakua na interest na mwenzie tu tena mara nyingi huwa ni sisi wanaume.....
No comments:
Post a Comment