Aliyekuwa Mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Aslay Isihaka maarufu kama Aslay, Tessy Chocolate amethibitisha kumfutilia mbali staa huyo tangu Penzi lao lilipoisha.
Miezi michache Baada ya Penzi hilo kufika mwisho Tessy Chocolate Amedai kwamba kwa sasa hapotezi muda wake kumuwaza mwanaume huyo, kwani ameshamsahau na sasa ana maisha yake mengine.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Tessy alisema kuwa alipata shida mwanzoni lakini tangu agundue kwamba msanii huyo hakuwa chaguo lake aliamua kuishi maisha yake.
Nilipata shida sana mwanzoni, kila mtu alikuwa ananishauri anavyojua yeye, lakini nashukuru Mungu siku zilienda na sasa hivi nimeshamsahau kabisa.
Kilichobaki kati yetu ni kumlea tu binti yetu Moza basi, pia sidhani kama naweza nikarudi tena kwake nina maisha yangu na ninayafurahia”.
Aslay na Tessy walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi na wakafanikiwa kupata Mtoto mmoja wa kike anayejulikana Kama Mozah.
No comments:
Post a Comment