Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameeleza maoni yake baada ya kusikia Edward Lowassa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).
Sumaye amesema “Mimi haunipi shida, mtu akiamua kuhama chama na kwenda kingine ni uamuzi wake,” alisema Sumaye.
“Kama kaamua acha aende, sisi tutaendelea kujenga chama na hicho unachokisema cha kuhama ni ndoto ambayo haipo,” amesema Sumaye alipoulizwa kama na yeye ni miongoni mwa watakaorejea CCM.
Edward Lowassa alijiunga CHADEMA Julai 2015 baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mchakato wa kutafuta mgombea wa Urais ndani ya CCM.
No comments:
Post a Comment