Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ,Edward Lowassa amerudi katika Chama chake cha zamani cha CCM akitokea CHADEMA, Lowasa alihama CCM na kujiunga na CHADEMA mwaka 2015.
“Ndugu zangu kama alivyozungumza Lowassa ametumia maneno mafupi amerudi nyumbani na nyumbani ni hapa CCM, ndio maana amesimama kwenye jengo la Makao Makuu Ofisi ndogo ya CCM,” Rais Magufuli amesema.
Shughuli ya kumpokea Lowassa imehudhuriwa na wanachama mbalimbali na wananchi wachache waliokuwapo.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema, “Ametangaza kurudi nyumbani na tuko tayari kumpokea.”
Edward Lowassa alijiunga CHADEMA Julai 2015 baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mchakato wa kutafuta mgombea wa urais ndani ya CCM.
Muya
ReplyDelete