Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima amefika nyumba kwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media (CMG), Ruge Mutahaba kutoa salamu za pole kufuatia msiba wake.
Mwili wa Ruge Mutahaba utawasili leo nchini kutoka nchini Afrika Kusini. Atazikwa nyumbani kwao Bukoba siku ya Jumatatu.
“Kufa ni njia ya kwenda mbinguni, hakuna mtu anayekwenda mbinguni akiwa na mwili huu namna pekee ya kwenda mbinguni ni kupitia kuuvua mwili kwa namna ya kimwili wale wanaoachwa ni tukio la masikitiko sana lakini kwa namna ya Rohoni ni tukio la faraja amekwenda mbinguni,” Askofu Gwajima.
Ruge Mutahaba amefariki siku ya February 26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.
No comments:
Post a Comment