Wazazi, tamaa za kuongeza mahari zitapelekea binti zenu kuzeekea nyumbani - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 25, 2019

Wazazi, tamaa za kuongeza mahari zitapelekea binti zenu kuzeekea nyumbani



Binti anataja mahari yake pesa kiduchu sababu anamuonea huruma mpenzi wake, hataki kumkomoa lakini nyie wazazi mnakuja kuongeza mara nne zaidi. Huo ni upumbavu wa kiwango cha juu kabisa.

Kwani wewe ndiye unayeenda kuolewa au kuvumilia kero za ndoa!? Au unataka fidia kwa malezi ya mtoto wako? Je, unafikiri utaweza kupata fidia ya malezi yako kwa mtoto hata ukipewa milioni 50?

Nikimuoa mwanao kwa pesa ndogo itanipa nguvu ya kukusaidia mkwe wangu kila unapokuwa na shida. Kama naishi na mwanao miaka kumi na zaidi je, unahisi utakula pesa yangu kiasi gani ?

Sasa ni hivi, tunawaomba wazazi mjue kuwa mnatupa kero kubwa sana sisi waowaji hasa sie tunaoishi maisha ya tabu sana. Wengine pesa tunazipata kwa shida sana jamani, mambo hayo muwe mnaangalia na mtu wa kumfanyia.

Wale wenzetu walio katika neema za kazi nzuri au biashara nzuri sio tatizo kwao, ila sie wabangaizaji mnakuwa kama mnatukomoa tu yani.

Unakuta familia nyingine ni za kidini kabisa lakini bado wanafanya ujinga wa hivi, hiyo dini inakuwa wapi sasa?

Kwa sisi waislam mtoto wa kike ndio anayesema mahari yake, hilo tunalijua. Sasa lile ongezeko lingine la nini tena jamani? Wewe baba na wewe unataka mahari ya nini tena? Bibi na mama mkwe na nyie mnataka mahari ya nini tena jamani?

Mkiendelea na tabia hii hao watoto wenu watazeekea majumbani kwenu. Ndoa zenyewe siku hizi zimekuwa za kutest, miezi sita tu kila mtu kivyake halafu unataka mahari ya milioni kwa mtoto wako?

Wengine wanataka milioni mpaka tatu wengine tano mpaka kumi. Muwe na huruma jamani, maisha ya sasa sio malaini tena, pesa tunaipata kwa tabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages