Duh! Inasikitisha sana.
Chukulia kwamba enzi hizo ulikuwa ukisaka mke, hatimaye ukamuona binti ambaye kwa akili yako na moyo wako uliamini yeye ndiye tumaini la maisha yako, yeye ndiye haswaaa ktk safari ya maisha yako (yaani mke stahili kwako). Bila kusita ulimuelewesha, naye (binti) akakubali. Watu weweee, full mzuka. Hatimaye salamu zikawafikia wazazi wa binti, wazazi wa binti wakakubali na kisha kukupangia Maali yenye jumla ya Tshs 3,000,000+. Bila ajizi wewe (mume) unajipiga piga kwa kuwashirikisha wazazi wako ili wakusaidie sehemu ya gharama za maali, wazazi wako wanauza ving'ombe ili kukupa msaada. Hatimaye mnafanikiwa kulipa gharama hizo na kisha kukabidhiwa mke na baraka za ndoa juu yake.
Mnaanza maisha, kipato cha maisha yenu ni kuhangaika huku na kule. Baada ya miaka kadhaa ya ndoa, mnabahatika kuwa na watoto wawili, lakini unagundua tabia za mkeo zinaanza kuwa tata. Unaamua kukausha kwa kuwa hujui kitu kinachoendelea kwa mkeo.
Mwisho wa siku baada ya malumbano ya kila Siku na mkeo (baada ya Tabia zake kubadilika) unagundua kwamba kumbe kuna bwanyenye flani hivi-mchimba madini kutoka Kankonko-ndiye chanzo cha mgogooro wa ndoa yenu. Baada ya kumbana sana mkeo kujua ukweli, ndipo anaamua kufunguka kwamba;
"Ni kweli, nina mume wangu kutoka Kankoko ndiye anataka kunioa. Nilimkubalia anioe kwa kuwa nilijiridhisha kabisa yeye ndiye anayekidhi ndoto za maisha yangu, yeye ndiye anayekidhi vigezo vya mahitaji yangu, yeye ndiye mwandani wa sifa zangu". Anakazia;
" Samahani, nilikukubalia wewe kwa kuwa kipindi kile sikuwa na jinsi zaidi ya kutaka kujiegesha tu kwako sababu haukuwa unafanana na mimi, haukuwa na vigezo vya kuishi na Mimi. Sasa nimepata mume mwenye sifa nazozitaka".
Wakati akiendelea kufunguka hivyo, wewe (mume) unazidi kuchachawa, unapagawa sababu ndiyo unajua "huna chako". Unamuuliza " unachokiongea unamaanisha kweli?"..... naye anakujibu "serious kabisa" kisha anapigilia msumari kwamba "tena kanipa kabisa pesa ya kukurudishia maali uliyolipa, ikiwa ni pamoja pesa ya nyongeza kama usumbufu kwako ambazo jumla yake ni Tshs 10,000,000/=". Anachukua kipima joto (begi) chake na kuzitoa pesa na kisha kuziweka mezani.
Wakati anafanya yote hayo, wewe ( mume) unajaribu kupiga moyo konde, unajikaza kiume lakini inashindikana hatimaye unazimia, watoto wanakuja kukupepelea na hatimaye unazinduka, unamuona mkeo kwanza ndiyo hata hajari. Unamuuliza tena mkeo " are you serious? " naye mkeo anakujibu "yeah, am more than serious" unazimia tena kwa mda flani.
Wakati unazimia kwa mara ya pili, mkeo ndiyo anatumia nafasi hiyo kukusanya kilicho chake, unakuja kuzinduka unamuona mkeo na mabegi alafu anakuaga "bai bai, nakwenda kwa mume wangu, ubaki salama". Baada ya kugundua mkeo hatanii, basi wewe unaamua " ufe tu" kisha "unakufa" mkeo hajali na anaona kama unamchezea vile. Anaamua kuchukua karatasi na peni anaandika maneno haya " acha kujifanya unazimia zimia, mimi ndiyo naondoka hivyo. Sitaki uje unisumbue na mme wangu mpendwa, nakuachia watoto uwalee vizuri". Kikaratasi hicho anakuwekea kwenye paji la uso akitaraji ukizinduka tu, basi unakutana na meseji hiyo nzito, kumbe wewe umeshakufa hivyo......
Ndg, life is not fair, na pia maisha ya ndoa wakati mwingine yanakufanya uwe chizi, hususani ukiangukia sehemu isiyo sahihi.
Note.
Wengi mtafikiri nimeandika kuwafurahisha tu kama bongo movie vile, lakini ni kisa cha kweli kilichotokea huku mkoani. But jamaa hakufa (nimenogesha tu), ila machungu ya moyo ndiyo mpaka sasa anayaugulia, na mke ndiyo kasepa hivyo. Watoto kawapeleka kwa bibi yao. Yeye jamaa yetu kaamua kuchange life style ya ulevi tu kwa kwenda mbele, ambapo akitoka kwenye vibarua vya mia mbili mia mbili ujira anaoupata yeye ni pombe tu, pombe na yeye. Nilikuwa na mengi ya kusimulia mkasa mzima, lakini nimeona nisiwachoshe.
No comments:
Post a Comment