Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, karibu wanawake tisa kati ya kila kumi wanaridhishwa na maumbile ya sehemu za siri za waume au mabwana zao.
Kwa hiyo, ni mmoja tu kati ya wanawake kumi ambaye haridhishwi na saizi ya maumbile ya mpenzi wake.
Hii ina maana kwamba, ni wanawake wachache sana wasioridhishwa. Lakini, hawa wapenzi wao ni wale ambao kweli wana maumbile madogo kupindukia, ambao idadi yao ni ndogo sana.
Kinachofanya wanaume kupanga foleni kwa waganga kutaka kuongezewa ukubwa wa maumbile yao, ni kutokana na kutojiamini kwa wanume hao.
Lakini lipo tatizo lingine, je ni lipi?
Wanaume wenye tatizo hili linalofahamika kitaalamu kama small-penis syndrome, wanakabiliwa na wasiwasi kwamba sehemu zao za siri ni ndogo, wakati wala sio ndogo, lakini wanaume hao kwa bahati mbaya huamini hivyo.
Kama nilivyosema awali, kuna wanaume wachache sana wenye maumbile madogo kuliko kiasi, hali ambayo hufamika kitaalamu kwa jina la kubeza la micropenis. Hawa wenye wasiwasi wa kimaradhi, huaminikwamba, nao wako hivyo yaani maumbile yao ni madogo kuliko kawaida, wakati si kweli.
Wastani wa maumbile yaliyowima ni urefu kati ya inchi 5.5 hadi inchi 6.2. wale ambao wana maumbile madogo ambayo hayawezi kukidhi utashi wa mwanamke wanakuwa na maumbile ya wima ya urefu wa chini ya inchi 2.75. kumbuka nimesema maumbile wima, bila shaka mnanielewa vizuri.
Ni wanume wachache sana wenye tatizo hili, lakini karibu wanume watano kati ya kila kumi wangependa kuwa na maumbile makubwa, bila kujali maumbile yao ya sasa hivi. Hii ni dunia nzima siyo hapa nchini tu.
Hebu naomba mjipime kwanza kabla hamjaingia kwenye ujinga wa kudhani kwamba maumbile yenu ni madogo au hayawatoshelezi wake au wapenzi wenu
No comments:
Post a Comment