Ukimuamini mpenzi wako na kupuuza maneno ya watu, mtadumu milele - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 7, 2019

Ukimuamini mpenzi wako na kupuuza maneno ya watu, mtadumu milele



Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndio maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kulizungumzia. Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. Kwenu ninyi mlio katika mapenzi, aidha ya ndoa au uchumba, kwanza yawapasa mfahamu kitu mapenzi ni tunu au zawadi, mimi niite maalum kutoka kwa mola wetu. 

Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani katika maisha yetu, hivyo kwa wale wanaoyachezea chezea na kuyavuruga mapenzi kwa makusudi kwa kuumiza hisia za wenzao na kuwasababishia vilio vya simanzi si watu wa kupendeza kabisa mbele ya macho ya wale wanaojua hasa nini maana ya mapenzi. Sasa nikirudi katika kile nilichodhamiria kukiandika wiki, nazungumzia mambo mawili yanayokwenda sambamba ambayo endapo utayazingatia, yanaweza kuwa ni yenye manufaa katika ndoa na hata uhusiano wako wa kimapenzi. 

Moja miongoni mwa hayo mawili ni hili la kutosikiliza maneno ya watu. Ukae ukijua kwamba, wapo watu wasiopenda kuwaona wenzao wakiwa katika ndoa au uhusiano wenye furaha na amani. Watu hawa ndio wanaosababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi huku wapenzi wengine wakiachana wakiwa bado wanapendana. Maneno ya watu ndiyo yamekuwa yakijenga ama kubomoa ndoa nyingi hivyo basi sikushauri usiyasikilize kabisa ya watu, kuna mambo mengine ambayo unaweza ukaambiwa na watu yakakusaidia sana katika maisha yako. 

Wapo watu ambao wanaweza kukuhabarisha juu ya mambo mbalimbali, si vizuri ukawapuuza, wasikilize na pima maneno yao, angalia kama yanaweza kukusaidia ama laa. Ila sasa, kwa mfano anakuja mtu na kukuambia amemuona mumeo ama mpenzi wako na mtu mwingine, mtu huyu utamchukuliaje? Je anakuambia kwa nia njema au anafanya hivyo ili muachane afurahi? Endelea kujiuliza kwamba, endapo mkiachana yeye aliyekuletea taarifa hizo atafaidika na nini? Kwa kifupi hakuna. 

Ndio maana nasema, nayoambiwa na watu yachuje kwanza kabla ya kuyafanyia kazi sio kila unaloambiwa unakimbilia kuchukua uamuzi. Maneno ya watu mara nyingi sana yanasababisha kuvunja ndoa za watu wengi sana kama sio kusasabisha machafuko katika ndoa hivyo ni vyema ukaepukana nayo. 

Hata hivyo, utaweza kuepukana nayo kama tu utakuwa unamuamini mpenzi wako. Uaminifu ni kitu cha msingi sana kwani unaposhidwa kumuamini mwenza wako mara nyingi sana utakuwa ukidhani kwamba anakusaliti hata kama unavyodhani au kuambiwa na watu vinaweza vikakosa ukweli. Hali hiyo inaweza kukufanya ukakosa raha kila mwenza wako anapokuwa mbali na wewe. Si kukosa raha tu anapotoka ama anapokuwa mbali na upeo wa macho yako bali pia anaporudi unaweza kushindwa kuonesha upendo wako kwake na kuweza kujenga chuki dhidi yake. 

Ni wachache sana ambao ni waaminifu kwa wanandoa wenzao. Wengine wakipewa maneno ya uongo tu kwamba mwenza wake ana uhusiano na mtu mwingine anakubali mara moja hata kama habari hizo hazina ukweli wowote, matokeo yake unachukua hatua ambazo zinaweza kuteteresha penzi lenu. 

Amini kwamba mwenza wako ni mwaminifu kwako na jijengee mazingira ambayo na yeye ataamini kwamba wewe ni mwaminifu kwake. Muamini ili naye akuamini. Epuka sana kufanya mambo ambayo yanaweza kumsababishia mwenza wako akadhani una uhusiano wa kimpenzi na mtu mwingine. Waweza kufanya hivyo kwa kuwa makini na maneno yako pamoja na matendo yako ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kudhihirisha kwamba sio mwaminifu katika ndoa. 

Kitendo cha kuchelewa kurudi kazini kila siku bila kuwa na sababu za msingi, kulala nje, kuwa na uhusiano wa karibu na watu jinsia tofauti bila kuwepo na sababu za msingi, kupunguza mapenzi, kutokuwa na heshima ni baadhi ya matendo ambayo yanaweza kuonesha kwamba sio mwaminifu hivyo ni vyema ukaepukana navyo​



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages