Miongoni mwa watu ambao wanatakiwa kupewa heshima zote hapa duniani ni wadada wa kazi za nyumbani ( house girl), maana hawa wamekuwa wana msaada mkubwa sana katika familia zilizo nyingi. Wamekuwa wakiwasaidia wenye nyumba katika kutimiza majumu mbalimbali ambapo mimi binafsi naamini kazi hizo wanazozifanya na wafanyakazi hao kama wenye nyumba wakipewa wazifanye ni lazima zitawashinda hii ni kutokana na ugumu na wingi wa kazi hizo.
Lengo la kuja hapa si kuwasifia wadada wa kazi ila nafanya hivyo kwa sababu najikuta naguswa sana na umuhimu wa wadada wa kazi katika kutekeleza majukumu mbalimbali wayafanyayo. Kama wewe ni mdada wa kazi na unasoma makala hii basi mwenyezi Mungu akautie nguvu kila wakati katika kutekeleza yaliyo mema na yenye kumpendaza bosi wako.
Baada ya kusema hayo naomba sasa naomba nilonge na wakina mama wote walioko kwenye mahusiano ya ndoa ambao wanaishi na wafanyakazi wa ndani.
Hivi uliwahi kujiuliza ni kwanini wanaume wengi hupenda kuwa na mahusiano na wasichana wa ndani? Kama hujawahi kujiuliza basi leo nitakupa ukweli usiojua kuhusu jambo hili.
Ipi hivi wanandoa wanapoingia katika mahusiano ya kimapenzi huwa kunakuwepo na upendo wa kweli baina yao mwanzoni kabisa mwa mahusiano hayo ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo upendo unavyozidi kushuka, jambo hili hutokea hii ni kwa sababu ya wanandoa hao hufika hatua wanazoeana sana hivyo kila mmoja wao kumuona mwenzake ni mtu wa kawaida sana hivyo kupelea kushuka kwa heshima baina yao.
Hivyo inapofika hatua ya kwamba wandoa hao wamezoea na heshima imeshuka hivyo ndoa hubadilika mwelekeo na kuwa chungu kama shubiri, na inapofika hatua hii mwanaume huwa haoni thamani tena ya mkewe.
Na kwa kuwa falsafa ya mahusiano inatuambia ya kwamba mwanaume huwa haitaji upendo kutoka kwa mkewe katika suala zima zima la mahusiano, bali mwanaume huhitaji heshima ya kutosha kutoka kwa mke wake, hivyo inapofika kipindi mwanaume huyo haoni tena thamani na upendo kutoka kwa mkewe hivyo anaamua kung`aza macho yake kwa mtu ambaye atampa heshima.
Na kwa kuwa wewe mkewe umebadilika kitabia haupo kama ulivyokuwa zamani hivyo mwanaume huyo anaamua kwenda kwa mfanyakazi wako wa ndani, kwa kuwa mwanaume anaona heshima nyingi kutoka kwa mfanyakazi wa ndani kuliko kwako.
Nini kifanyike ili kuzua tabia ya mwanaume kutoka kimapenzi na wafanyakazi wa ndani.
Mosi; ewe mwanamke ili mwanaume wako asiwe na tabia hii ya kuwapenda kimapenzi wafanyakazi wako wa ndani unatakiwa kuelewa ya kwamba kitu ambacho humpa mwanaume tabasamu mwanana la kimapenzi ni pamoja na kumuonesha mwanaume huyo heshima iliyo ya kweli na si vinginevyo.
Pia si kila jukumu anatakiwa kufanya mfanyakazi wako wa ndani mengine unatakiwa kufanya wewe mwenyewe, kila wakati kumbuka majukumu yako ni yapi na majukumu ya kumpa mfanyakazzi wako ni yapi pia.
Mbili; Mwanaume achana na tabia hii kwani haitakusaidia kwa chochote zaidi ya kujenga mahusiano yaliyo mabovu baina yako na mpenzi wako. Lakini pia Afisa Mipango nakushauri ya kuwa kila wakati ewe mwanaume unatakiwa kukumbuka kiapo chako cha ndoa.
Tatu; Ewe mfanyakazi wa ndani tafadhari sana achana mara moja na tabia hiyo ya kufanya unayajua sana mapenzi, kilichokupelekea hapo ni kufanya kazi na si mengineyo kwani kama utaendelea na tabia hiyo utaweka sumu kwenye familia hiyo. Muombe Mungu akupe na nawe kipenzi wa moyo wako.
Mwisho naomba nikutakie siku njema na majumu mema, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.
Na. Benson Chony
No comments:
Post a Comment