Mwanaume asiyeweza kufua chupi ya mpenzi wake hastahili kuivua
MWANDISHI mmoja maarufu wa habari za uchunguzi katika gazeti moja nchini Ghana ambaye pia ni mshindi wa tuzo katika nyanja hiyo, Manasseh Azure ameibua mjadala mkali miongoni mwa raia wa nchi hiyo kuhusu jambo linaloweza kuonekana kama nyeti baina ya wapenzi la wanaume kufua nguo za ndani za wapenzi wao.
Katika kitabu chake kipya kilichozinduliwa hivi karibuni kinachojulikana kama Letters to My Wife, mwandishi huyo anakiri kuwa ataosha nguo za ndani za mkewe iwapo itahitajika tena bila aibu.
Katika sehemu moja ndani ya kitabu hicho anasema, “Nitaosha chupi zako siku yoyote. Si mpaka uwe mgonjwa. Nitaosha chupi zako kwa furaha wakati wowote inapohitajika kufanya hivyo. Nitaziosha siku yoyote ya mwezi. Hilo ndilo jibu langu. Na ni ukweli uliotaka kusikia kutoka kwangu."
Akitetea uamuzi wake kufanya kitendo hiki ambacho wanaume wengi nchini humo kamwe hawawezi kufanya, Azure anasema: “Kuosha mavazi ya mpenzi wangu hakutapunguza ukubwa wa uume wangu. Hakutanipunguzia uwezo wangu kiakili. Hakunipunguzii chochote. Hivyo basi usiwe na wasiwasi kwamba ukiwa mgonjwa katika ndoa yetu, nitakusanya kila unachohitajika kufanya hadi utakapopata nafuu.
"Mimi ni mwanamume halisi, Serwaa. Niamini! Mwanamume ambaye hawezi kuosha chupi yako hastahili kukuvua chupi hiyo,” alisisitiza.
Katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho mnamo Jumatano wiki iliyopita, Manasseh alikiri kwamba wakati wa fungate yao, alifua chupi za mkewe ili kumsaidia ajiandae kwa haraka ili wawahi kwenye miadi waliokuwa nayo.
Rebecca Azure, mkewe Manaseh pia alisema ikiwa watu walidhani kwamba mume wake hakumaanisha chochote alichoandika katika kitabu hicho, wanapaswa wasubiri siku atakayosimulia hadithi ya ndoa yao.
‘Letters to My Future Wife’ ni mkusanyiko wa barua ambazo mwandishi huyo alimwandikia mkewe kabla ya kufunga ndoa na Rebecca Eduafo-Abraham.
Maudhui aliyoandika yalikuwa kwa kawaida maswala tata, ambayo huenda yakaimarisha au kuvunja mahusiano baina ya wapenzi wawili.
Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Christ the King auditorium jijini Accra, na hafla hiyo ilihudhuriwa na Second Lady, Mrs. Samira Bawumia, Dkt Joyce Aryee, Mheshimiwa Abla Dzifa Gomashie, Ace Ankomah miongoni mwa wageni wengine maarufu.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments:
Post a Comment