Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Msukuma amesema michezo ya kamari maaarufu kama kubeti imefanya kina baba wengi kushindwa kujali familia zao.
Msukuma amesema mchezo huo kwa sasa umekuwa kama uchawi huku hakitahadharisha kuwa ni chanzo cha umasikini.
"Kuna vitu vinaitwa kubeti, baba mtu mzima unaenda kubeti nyumbani umeacha jero hivi kweli unaweza kulisha mke na jero," amesema na kuendelea.
"Na ninyi kina mama ngoja niwaambie akikuachia jero, fanya akili akute umechoma kuku, akikulizamwambie nimetumia akili," ameeleza Musukuma.
Mbunge Msukuma aliwahi kugonga vichwa vya habari vilivyo mara baada ya kusimama bungeni na kutetea hoja yake ya kutaka serikali iruhusu matumizi ya bangi, kwani inaonekana kuwa msaada mkubwa kwa vijana.
No comments:
Post a Comment