Mambo 7 Ya Kumfanyia Mpenzi Wako Hii Valentine’s Day - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 11, 2019

Mambo 7 Ya Kumfanyia Mpenzi Wako Hii Valentine’s Day

Mambo 7 Ya Kumfanyia Mpenzi Wako Hii Valentine’s Day




Siku ya Valentine ndio hio imetufikia. Wengi wamekuwa wakiongea kuhusiana na hii siku. Siku hii kwa wale ambao wanaisherehekea wanadai ni siku ya wapendanao. Wengi huichukulia siku hii ni spesho kwa wawili wapendanao kujumuika pamoja.


Well, kwa wale ambao wanaisherehekea siku hii, ni mambo gani ambayo unayafanya? Wengi watakuambia wanangojea jioni wakakutane na wapenzi wao waende dinner. Wengine wangesema wanawanunulia wapenzi wao maua, wengine wanasema watawasha mishumaa wakati wa jioni ili kuleta mazingira ya mahaba, na baadhi watadai watabikiri watu siku hio.

Hapa Nesi Mapenzi tuna wazo tofauti. Wazo letu ni kuwa unafaa kuspend siku nzima na mpenzi wako. Kama unahitajika kazini ama masomoni, siku hii itenge spesheli kwako na mpenzi wako, yaani kuanzia asubuhi hadi usiku unapaswa kuwa na mpenzi wako. Chukua off kutoka kazini.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo unahitajika kufanya katika siku ya Valentine’s day.

#1 Anza na kiamsha kinywa ukiwa kitandani.

Kupata kiamsha kinywa kitandani ni jambo ambalo linaonekana kifahari. So anza siku yako kwa kuamka polepole ili usimuamshe mpenzi wako. Ingia jikoni umuandalie kiamsha kinywa ambacho anakipenda zaidi. Hakikisha ya kuwa ukishamaliza kupika unaosha vyombo vyote ili usimpe kazi yeyote atakapoamka.

Weka kiamsha kinywa kando yake halafu umuamshe polepole kwa kumbusu. Kama kuna ua ambalo ushalinunua tayari unaweza kumnukisha ili aamke na furaha. [

#2 Ogeni pamoja.

Baada ya kunywa kiamsha kinywa, ni wakati wa nyinyi wawili kuenda kuoga. Maji moto ni njia nzuri ya kuwachangamsha ili siku yenu iwaendee vyema. Kama mumezoea kuoga pamoja, unaweza kuleta utofauti wa kuoga, unaweza kumwambia, “bebi leo nataka nikusugue mgongo”

#3 Angalieni filamu.

Baada ya nyinyi wawili kuvaa nguo, ni wakati wa kukaa kwa kochi huku mnagusana. Wekeni filamu ya kimahaba ambayo nyinyi wawili mnapenda. Kama inawezekana, mnaeza kuenda katika sinema kuangalia filamu ya mapenzi ambayo bila shaka atapenda. Kumbuka ya kuwa lengo lako siku ya leo ni kumtosheleza mpenzi wako, na wala si kujitosheleza. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke apendezwe na wewe]

#4 Chamcha mle sehemu ya wazi.

Kula katika sehemu iliyowazi ina starehe zake. So baada ya kuangalia filamu, mpeleke mpenzi wako kula chakula cha mchana katika sehemu iliyo wazi. Unaweza kuenda katika mkahawa unaoujua halafu uagize sehemu ambayo unayaona mazingira kwa upana. Kama haitawezekana, unaweza kuchukua hatua ya zaidi kufanya picnic. Mpeleke sehemu ya hifadhi yeyote, tandika mkeka, toa vinywaji na chakula cha mchana. Bila shaka atafurahi.

#5 Hifadhi kumbukumbu ya siku hio.

Baada ya kuspend muda mkiwa pamoja na kukula chakula cha mchana, mnapaswa kurudi nyumbani. Usijisumbue kutaka kufanya mengi siku hii ya Valentines Day. Pia usiharakishe mambo, fanya mambo polepole na kwa utulivu. Wakati mkiwa nyumbani mnabarizi, toa kamera yako na uanze kuchukua video ya vitu ambavyo nyinyi wawili mmefanya siku hii. Kumbukumbu hizi mtaziweka na mtakuja kuzikumbuka miaka ya usoni. [Soma: Jinsi ya kumuomba mwanamke atoke out na wewe]

#6 Washa mshumaa.

Watu wengi huhusisha siku hii na uwashaji wa mishumaa. Hivyo nawe usiachwe nyuma. Agiza chakula kutoka nje na upange mishumaa kadhaa kwa meza. Kama haitawezekana, unaweza kumpeleka katika hoteli yeyote ambayo imetenga siku hii kuwa spesho kwa Valentine’s Day ili kusherehekea. Msithubutu kuruka hatua hii ya kula chakula cha jioni bila kuwasha mishumaa, hata kama nyote wawili mmechoka. Hatua hii ni muhimu kwa kuwa inaifanya siku nzima kuwa kamili.

#7 Na mwisho kabisa...

Mkishamaliza chajio, rudini nyumbani na mjitayarishe tayari ya kupumzika na kutomasana kwa kitanda. Kwanza mnaingia kuoga, tia vinywaji kidogo ili kuondoa kiu. Nendeni chumbani na mzime taa. Washeni mishumaa kadhaa chumbani na muinjoy usiku mzima kwa mlalano. Hakikisha usiku huu unakuwa bora zaidi kuliko usiku wowote ule.
Kivyovyote vile, mpenzi wako ataifurahia siku hii kwa kuwa atajiona spesho. Siku hii ukiipanga kama tulivyokueleza basi mpenzi wako atakushukuru na atafall na wewe zaidi ya vile ambavyo hukua unatarajia.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages