Kuwa na wapenzi wengi ni tatizo la kisaikolojia - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 9, 2019

Kuwa na wapenzi wengi ni tatizo la kisaikolojia



Katika ulimwengu wa sasa kuwa na uhusiano wa mapenzi na zaidi ya mtu mmoja ni kitu cha kawaida sana. Hapa nikilenga jinsia zote kuanzia wale walio ndani ya ndoa na ambao bado.

ILIVYOZOELEKA

Awali wanaume ambao kiasili huongozwa na tamaa ya muda mfupi ya kufanya mapenzi ndiyo pekee waliokuwa wakihusishwa na wapenzi wengi suala ambalo hata kisayansi linathibitishwa hivyo kutokana na utofauti wa maumbile kati yao na wanawake.

WANAWAKE WAMEINGIA

Lakini siku hizi hata wanawake nao hawapo nyuma. Wengi wao wamekuwa wakijiingiza kwenye uhusiano wa wapenzi zaidi ya mmoja kutokana na madai ya kuumizwa na wanaume wao ambao wamekuwa wakiwasaliti kila kukicha kiasi cha kushindwa kuwatimizia mahitaji kadhaa hasa suala la unyumba.

WASIOOLEWA PIA

Hata hivyo, tafiti zimeonesha kwamba, asilimia 78 ya wasichana wa kuanzia miaka 17 hadi 25 ambao hawajaolewa nao wamekuwa na kasumba ya kutotulia na mpenzi mmoja kwa kuwa huhitaji wanaume wenye uwezo kifedha ambao huwatimizia mahitaji yao na wakati huohuo wakitaka kuwa na wale wanaowapenda kwa dhati.

MADHARA YAKE SASA

Kusheheni wapenzi kuna madhara mengi ambayo yanafahamika, kama vile kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na Ukimwi, lakini kitu ambacho wengi hawakifahamu ni kwamba, kumiliki wapenzi wengi husababisha matatizo ya kisaikolojia. Hii ni kutokana na wahusika kukiuka hitaji la moyo la kuwa na mpenzi mmoja ambaye atamuamini na kuwa na lengo naye moja.

TWENDE NA TAFITI

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali ikiwemo ile ya wanazuoni kutoka Chuo cha Dunedin nchini New Zealand ya mwaka 2007, ilionesha kuna matatizo ya kisaikolojia yanayotokana na mtu kuwa na wapenzi wengi kama ifuatavyo:
Kushindwa kutosheka kihisia. Wengi kati ya watu wanaojihusisha na wapenzi wengi waligundulika kuwa na tatizo hili ambapo kawaida hata walipokuwa tayari wameshakutanishwa na wapenzi wao faragha bado walionekana kutamani kuwa na wapenzi wapya pale wanapokutanishwa na watu wapya iwe wanaovutia zaidi kuliko wapenzi wao au lah!
Tatizo jingine la kisaikolojia la wanaojihusisha na wapenzi wengi ni mwendelezo wa tatizo lililotajwa hapo juu ambapo mtu hujikuta akishindwa kutulia kabisa na mpenzi mmoja hata kama ataamua kufanya hivyo kutokana na majukumu.
Kama hiyo haitoshi, tatizo kubwa zaidi linalowakuta watu hao huwa ni ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa wanapokuwa na wapenzi wao kwa muda mrefu kwa kuwa akili yao huzoea kuwa na wapenzi wapya ambao huwasisimua zaidi kuliko wa zamani ambao huwafanya wakinai polepole.

HITIMISHO


Kwa hiyo kama wewe unajijua huwezi kuwa na mpenzi mmoja mpaka uwe na mwingine na kuzidi kutafuta mwingine, ujue umeshaathirika kisaikolojia. Cha kufanya ni kujifunga kwa dhati huku moyo wako ukijua ni ugonjwa na tiba yake ni kuachana na wapenzi wengi, baada ya muda utazoea.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages