KISA CHA BABA NA MWANAE; BABA NIMEMCHOKA MKE WANGU BORA TU KUACHANA! - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 7, 2019

KISA CHA BABA NA MWANAE; BABA NIMEMCHOKA MKE WANGU BORA TU KUACHANA!



Kila siku alikua anagombana na mke wake, alikua hana amani na kila mara alikua ni mtu wa kulalamika, kwakua nyumba haikua na amani na kwakua kwao ni karibu Jackson alikua akitumia muda mwingi kwao na kila wakati akiwa na kazi zake alikua anaona ni bora kucfanyia nyumbani kwao ili akirudi nyumbani tu ni kulala. Baba yake aliiona hiyo hali, siku moja alimuita na kumuuliza kwanini anakua hivyo, alimuelezea matatizo ya mke wake.

Alimuambia kuwa mkewe ana kelele sana, ana kisirani kiasi kwamba hawezi kuwa na amani kuna wakati anatamanio hata kuachana naye. Baba yake alimuambia subiri, kesho ukienda kazini muambie mke wako awe anakuja na kushinda na Mama yako hapa mpaka jioni. Walikua bado hawana mtoto hivyo Jackson hakuona shida sana,a limuambia mke wake. Lakini jioni aliporudi kwa Baba yake, Baba yake alimpa mfuko flani na kumuambia ampelekee mkewe.

Kila siku alifanya hivyo, asubuhi mkewe anatoka na kwenda nyumbani kwao na jioni Baba yake humpa mfuko ambao hata hajui una nini ndani ili kumpelekea mkewe. Alishangaa kuona mkewe anaabadilia, anafuraha, hana kisirani na anamchangamkia. Aliwaza sana lakini hakupata jibu, baada ya miezi miwili ana amani anatamani kuwahi kurudi nyumbani aliamua kumuuliza Baba yake alikua kafanya nini? Baba yake alitabasamu na kumuambia. Mke wako anapokuja kwangu haji kukaa tu, nimemtafutia kazi anafanya mpaka jioni.

Hii inamfanya kuwa bize, badala ya kutwa nzima kukuwaza wewe, kuwaza unafanya nini na kutamani urudi nyumbani, anauza duka hivyo yuko bize na wateja na kamaa ana kisirani chake basi anakimalizia kwa wateja na majirani hivyo ukirudi nyumba ina amani. Jackson alishanga ana kumuuliza vipi kuhusu ule mfuko unaonipa unakuaga na nini? Baba yake akasema, unafikiri una cha maana basi, sansasana ni karanga na Biscuit na vipipi.

Wanawake wanapenda kujaliwa, unapomletea zawadi hata mara moja moja anajua kuwa pamoja na ubize wako kazini lakini ulikua unamuwaza yeye muda wote hivyo unampa amani kwa kumuonyesha kuwa anajli, unamuondolea kisirani kwani mwanamke akishaolewa huamini kuwa amebadilika, amekua mbaya na hapendwi tena hivyo ni kazi yako kumuonyesha kuwa ana thamani na unampenda kama zamani.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages