Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la William Saimon, mkazi wa Bihawana, Jijini Dodoma anatuhumiwa kuhusika na tukio la kumkaba na kumbaka bibi kizee mwenye umri wa mika 77.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma amesema februari 11, 2019, saa 5: 55 usiku, bibi kizee aliyejulikana kwa jina la Jema Macheho (77) amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma baada ya kukabwa shingo kisha kubakwa na kijana huyo pamoja na wenzake vijana wengine wawili.
Kwa mujibu wa Kamanda Muroto, mtuhumiwa mmoja tayari ameshakamatwa na wenzake wawili bado wanaendelea kusakwa kwaajili ya kuwafikisha katika vyombo vya dola.
Aidha katika tukio lingine Kamanda Muroto amesema watu wengine wakiwamo raia wa China wamekamatwa wakiwa na mashine 68 za kuchezeshea kamari maeneo mbalimbali ya mkoa huo zilizohifadhiwa katika baa, maduka, grocery na vituo vya usafiri.
Kamanda Muroto amewatahadharisha wananchi wa mkoa wa Dodoma kuepukana na uhalifu kwani hakuna mtu ambaye atabaki salama kwakuwa uhalifu haulipi.
Tuesday, February 12, 2019
Kijana ambaka na kumuua bibi wa miaka 77 Dodoma
Tags
# Mapenzi
Share This
About Utundu Kitandani
Mapenzi
Labels:
Mapenzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment