Je, ni sahihi mke wangu kuniambia kila Mwanaume anayemtongoza? - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 3, 2019

Je, ni sahihi mke wangu kuniambia kila Mwanaume anayemtongoza?



Nimevurugwa sana..

Boss wa mke wangu anamtongoza mke wangu kwa uchu sana kiasi kwamba hadi nimeanza kupoteza matumanini.

Mke wangu hana raha kabisa wafanyakazi wenzake wanammendea na boss wake naye humohumo yani wapo msululu.

Imefika hatua boss wake ameanza kutafuta safari za kikazi ili asafiri na mke wangu lengo lake ni kumbandua mke wangu na wote tunafahamu kwasababu mke wangu ananiambia kila kitu, kila ujumbe anaotumiwa na kila mazingira magumu anayokutana nayo(wanaume mnanielewa hapa)

Nifanyaje wandugu nataka kumsaidia mke wangu asinase kwenye mtego wa huyu simba.

Je nimkataze asiwe ananiambia habari za kutongozwa na wanume?

Wanaume wenzangu mnaishije na wake zenu walio ajiriwa sehemu mbalimbali,mnakutana na changamoto zipi kwenye ndoa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages