JE KUCHUNGUZA SIMU YA MPENZI WAKO NI SAHIHI AU UJINGA? - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 28, 2019

JE KUCHUNGUZA SIMU YA MPENZI WAKO NI SAHIHI AU UJINGA?

JE KUCHUNGUZA SIMU YA MPENZI WAKO NI SAHIHI AU UJINGA?



Penzi lilojaa furaha na lenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kwa wengi ni kitendawili kigumu sana. Na kwa sehemu kubwa ugumu huo hutokana na ukosefu wa uwazi na ukweli.KUKOSEKANA kwa mazingira ya uwazi na ukweli  husababisha ubinafsi wa hali ya juu  ambao ukiachiliwa kuendelea hufikia kiwango cha ukatili tunouona katika usaliti na vifo vya mahusiano mengi.Kwa wenye magari ili gari lako liweze kudumu muda mrefu unaagizwa kuangalia kiwango cha maji na oil katika gari yako mara kwa mara na kushindwa  kutii agizo hilo gari lako halitaweza kudumu. Katika mahusiano ya kimapenzi kwa wale wenye malengo ya muda mrefu kuhakikisha kuwa mpenzi wako ni wako peke yako ni jambo la msingi katika ulimwengu huu wenye michepuko ya kila rangi. Tafiti nyingi zinaoonyesha kuwa mahusiano yenye uwazi wa kiwango cha juu yanakuwa na furaha zaidi na hudumu kwa muda mrefu sana ukilinganisha na mahusiano yenye mazingira ya usiri na ubinafsi.
Uwazi unasaidia kumfahamu mpenzi wako vizuri zaidi na hivyo kuwez kumsaidia katika maeneo yenye mapungufu au udhaifu kwa kuwa hakuna aliye makamilifu mara nyingi udhaifu usipogunduliwa mapema majanga hujitokeza. Kuna mambo mengi yanayochangia kufa kwa uhusiano na usaliti ni moja kati ya mambo makuu katika hayo. Ili kuweza kuepuka moja kati ya mambo yanayosababisha usaliti ni vyema kuangalia upya matumizi ya simu kwa uangalifu sana kwani  matumizi mabaya ya simu yamewaletea wengi majanga. Simu ni chombo kizuri ambacho kinaweza kuchangia katika kuboresha penzi na kulinda penzi. Kwa kuwa simu hutumika sana katika kuanzisha na kuendeleza usaliti upo umuhimu wa wapenzi kupeana uhuru wa kupekuliana simu zao bila hofu yoyote.Watu wengi wanapingana na hilo  jambo ambalo linathibitisha kuwa mahusiano mengi hayana amani ya kweli.KUMBUKA KUWA HUWEZI KUWA NA AMANI YA KWELI KAMA HUNA UHURU.Mfungwa hata awe kwenye gereza la dhahabu na kula chakula kwenye sahani za dhahabu ha hata akiende chooni na choo kikawa cha dhahabu kwakuwa hana uhuru hana raha kabisa.Kwanini uendelee kuwa katika uhusiano ambao hauna uhuru?Ni wakati wa kufurahia maisha sio kuishi kwa kuvumiliana,upo umuhimu wa kutumbua majipu ili furaha na maendeleo ya furaha yaonekane.
Moja kati ya dalili ya kwamba mpenzi wako ana mpango wa kukusaliti au tayari amekwisha anza usaliti ni kudai kuwa simu yake ni yake binafsi na  hakupi uhuru  wa kuipekua. Dalili ya pili ni ile mpenzi wako anaposhindwa kutoa maelezo yalionyooka juu ya mahali alipokuwa au alipo mbali na  masaa ya kazi.Dalili ya tatu ni kuwa na ukaribu wa kimaongezi na mtu wa jinsia tofauti na yake. Dalili ya nne kupunguza kiwango na wingi wa uchezaji awa ngoma ya wakubwa. Dalili ya tano ni hapendi kukaa na mpenzi wake kwa maongezi kwa muda mrefu na mawasiliano ya simu ni machache. Iwapo wewe humpi mpenzi wako sababu ya kuwa na wasiwasi na wewe katika maeneo  hayo huna saababu ya kuhofia pale mpenzi wako anavyopekua simu yako.
Tafiti iliofanywa na shirika la ulinzi kwenye mitandao ya internet inasema kuwa asilimia 46 ya wake kwa waume hupekua simu za wapenzi wao. Mtu huanza kupekua simu yako pale aonapo dalili kuwa penzi kati yenu limepungukiwa furaha na msimsimko uliokuwepo mwanzoni na mpenzi wako anapoanza kupekua simu yako anatafuta jibu ya hali hiyo mbaya.
Kwanini watu hupekua simu za wapenzi wao na kwa nini wengine hawataki wafanye hivyo?
Hebu angalia hili, iwapo wewe ni mmoja wapo wa wale wasiotaka kupekuliwa simu zao. Mpenzi wako akapekua simu yako na asikute lolote baya si atajiona mpumbavu? Je, na pia akiacha kupekua  simu yako  na baada ya miaka miwili anasikia umempa mimba mfanyakazi mwenzio pia si atajiona mjinga na mpumbavu? Atajiona mpumbavu kwa kuwa kama angekua anapekuwa simu yako mapema angegundua  mapema?HALI kama hiyo imemkuta dada mmoja  baada ya kugundua kuwa  mtu aliekuwa anaamini kuwa mume mtarajiwa tayari alikuwa na mke na hapo hapo alikuw ni mjmzito.INAUMA sana mtu kukupotezea muda wako na hukuwa na uwezo wa kugundua kuwa unadanganywa.SIMU INAKUPA UWEZO HUO.
Ukweli ni kwamba kutokana na udhaifu wa kibinadamu iwapo mtu ataachiwa kufanya kama anvyopenda upo uwezekano mkubwa wa kufanya mambo mabaya yatakayowaumiza wengine na ndio maana kuna polisi na mahakama. Ukitaka kupingana namimi kuwa upekuaji wa simu ya mpenzi wako sio kitu kizuri naomba uangalie yafuatayo. Je, hujawahi kusikia viongozi wakubwa wa serikali wamefanya mambo mabaya? Hujawahi kusikia viongozi wa dini wamefanya mambo mabaya? Je, watu ambao wanakamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani wote ni vichaa au ni watu wenye heshima zao ukiwaona katika hali ya kawaida? Bila shaka hapo utapata ushahidi kuwa ipo haja kubwa ya kulinda uhusiano wa kimapenzi na kupekua simu ya mpenzi wako ni moja kati ya njia nzuri ya ulinzi huo .Tafiti zinaonyesha kuwa asilimi 60 ya wanandoa wameshawahi kusaliti na hiyo ni idadi kubwa na maumivu kwa yule asie na hatia ni makubwa sana. Hata kama hakuna dalili za usaliti, kumpa uhuru mpenzi wako kupekuka simu yako ili ajiridhishe ni jambo la muhimu kwani inakusaidia wewe uanepekuliwa kuongeza bidii kuendelea kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na kupiga vita vishawishi vyote vinavyotokeza. Kutokana na ukweli huo ni vyema mfanye kupekuliana simu kama mchezo uletao burudani kati yenu badala ya hasira.
Mkiweza kueleweshana juu ya mchezo huo na kupeana kanuni za mchezo huo kupekuliana simu hakuwezi kuwa tishio kabisa. Iwapo utafanya jitihada za kuonyesha penzi motomoto kwa mpenzi wako utampunguzia mpenzi wako haja ya yeye kupekuwa simu yako. Usimseme vibaya mpenzi wako kwa kupenda kupekua simu yako mara kwa mara mthibitishie kuwa unampenda na huwezi kumsaliti kwa kumpa uhuru wa yeye kupekuwa simu yako.Huoni kuwa hiyo ni njia rahisi ya kumthibitishia uaminifu wako Yule umpendae?NDIO  unaweza klusema kuwa atakuwa anafuta meseji zake, sawa hilo lipo lakini  iko siku atajisahau na atatumbukia mtegoni.
 Iwapo unajitahidi kuondoa sababu zote ambazo zinamfanya mpenzi wako awe na wasiwasi utaleta amani na furaha kati yenu badala ya migogoro. Unajua nini? Hata kama mpenzi wako atakuta mambo ambayo wewe unayaona ya utani wa kawaida lakini kwake yakawa yanamletea wasiwasi ichukulie hiyo kama fursa yakuelewa udhaifu na uelewa wa mpenzi wako na niwajibu wako wewe kumsaidia mpenzi wako katika hayo bila ya kuonyesha dharau yoyote au ukali wowote ule. Hata kama utakuwa umefuta meseji zote zile ambazo unaziona kuwa zina uwezo wa kuleta hali ya kutoelewana lakini pale unapompa mpenzi wako uhuru wa kupekuwa ile hofu ya kwamba huenda kuna meseji ulisahau kuifuta  itakusaidia wewe kuona jinsi gani usaliti ni wa hatari katika uhusiano wenu iwapo kweli unampenda mtu ulie nae. Iwapo kweli unampenda mtu ulie nae hakuna gharama ilio kubwa itakayokushinda kuitoa kwa ajili yake. Iwapo humpendi  mpenzi wako huwezi kuona hatari ya kumuumiza au kumpoteza mpenzi wako lakini iwapo unampenda utajiona kuwa unao wajibu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa mpenzi wako ana amani na wewe wakati wote.
Hebu fikiria, je kuna njia gani rahisi ya kumkamata mpenzi wako anapokuwa amechepuka na kuwa na mtu mwingine kimaapenzi zaidi ya simu? Kama hiyo ni njia rahisi kwa nini isitumike kulinda penzi mnalolithamini?Mtu anaekataa kutumia simu kama njia ya kulinda na kutunza penzi hana mapenzi ya kweli.
Wengi hutumia kisingizio kuwa kupekuwa simu ya mpenzi wako ni sawa na kuingilia uhuru wa taifa jingine, sio kweli kabisa kwani iwapo naweza kuzishika sehemu zako za siri  kwa uhuru wote ni sahihi kabisa kwa mimi kuwa na haki ya kujua siri zako zote zilizomo kwenye simu yako. Kinyume na hapo ni kudaganyana kabisa. Unajua nini? Kwa sababu yoyote ili mpenzi wako anapoanza kuwa na wasiwasi na wewe ni wajibu wako wewe unaedai kuwa unampenda kumsaidia kuondoa wasiwasi huo.Wasiwasi wake hauwezi kuondoka wenyewe bila ya wewe kumsaidia. Na kama huwezi kumsaidia katika hilo ni dhahiri  kuwa humpendi hata kama unampa mamilioni ya pesa kila siku. Kwa watu ambao hawajawahi kusalitiwa hawawezi kuona ukubwa wa wasiwasi  wa kuwepo kwa uwezekano wa kujeruhiwa  kama wale ambao ambao walikwasha salitiwa huko nyuma.Watu ambao wameshawi kuumizwa na usaliti au kuona marafiki zao wa karibu wameumizwa wanakuwa na wasiwasi mkubwa sana na ni wajibu wa wapenzi wao kuelewa chimbuko la wasiwasi huo.
Watu wengine wanajifariji kwa kusema kuwa sitaki kupekua simu ya mpenzi wangu kwani inaweza kuniumiza vibaya na hivyo kuepuka maumivu wanaogopa kushika simu za wapenzi wao. Huo ni umpumbavu kwani ni sawa na kusema kuwa “Nakuruhusu unisaliti lakini sitaki kujua kama unaisaliti”.
Unaposema hivyo na kukubaliana na hilo moja kwa moja unapoteza haki ya kuuliza maswali pale mpenzi wako anapokuwa amechelewa kurudi nyumbani, huna haki ya kuuliza swali lolote pale simu yako isipopokelewa au unapokuta simu ya mpenzi wako imezimwa . Je hapo kuna  mazingira ya furaha katika uhusiano huo? Haiwezekani kuwa na furaha kwa kuwa unayo maswali halali lakini ukiuliza mwenzio nakuwa mkali na kutoa maneno mabaya. Usishangae kuona hali kama hiyo kwani kwa wewe kuogopa kusisitiza uwazi kati yenu mpenzi wako ameingia kwenye mahusiano mengine ambayo anayathamini zaidi ya wewe.
 Hivi karibuni dada mmoja mzuri mwenye kazi nzuri alinisikitisha kwa kuniambia kuwa anatembea na mume wa mtu ambae anataka ampeleke akamtambulishe nyumbani kwao. Dada huyo  anadai kuwa mume wa mtu anampenda kwa kuwa anaweza kukaa kwake hadi saa nane za usiku na umuulizapo kuwa mbona muda umekwenda sana mkeo hatakushambulia. Dume hilo linamjibu kwa kumwambia “wewe nione kama vile sina mke na wewe ndio mke wangu “ Dada huyo mwenye elimu nzuri ameamini maneno hayo bila kutambua kuwa mwanaume huyo anamuonyesha ni jinsi gani alivyo mkatili na sio kuwa ana upendo mwingi.Kama anaweza kukaa na mwanamke mwingine hadi saa 8  za usiku bila kujali maumivu ya mkewe anafikiria ukatili huo hautafika kwake yeye? Usidanganyike sisitiza penzi la kweli na lenye uwazi mkubwa.
 Hebu fikiria, lipi bora, kugundua kuwa mpenzi wako anakusaliti au kugundua kuwa amekuambukiza UKIMWI? Kama ungejua kuwa kupekua simu ya mpenzi wako kungekuepusha na ugonjwa wa UKIMWI usingefanya hivyo kwa bidii zaidi? Lipi bora, upekuwe simu ya mke wako na ugundue kuwa ni msaliti au uje ugundue kuwa mtoto ulieamini kuwa wewe ndie ulisababisha ujauzito sio mototo wako bali ni wa mwanaume mwingine ( mkemia mkuu wa serikali anasema zaidi ya asilimia 40 ya watoto wanawaita baba watu ambao sio baba zao).
Simu ni kama moto, moto ukiutumia vizuri utachangia katika kufanya maisha yako yawe matamu zaidi lakini ukiutumia vibaya unaweza kuleta majanga. Kwa hiyo basi kwa kadri tunavyokuwa waangalifu katika matumizi ya moto lazima tuwe waangalifu katika matumizi ya simu. Hebu jiulize maswali yafuatayo.
1.     Je, kuna mambo ambayo hupendi mpenzi wako ayakute kwenye simu yako? Kwanini hutaki ayaone?
2.     Je, unapokuwa mbali na simu yako na ukawepo uwezekano wa mpenzi wako kusoma yaliyomo kwenye simu, je unakuwa na wasiwasi kuwa huenda mtu mwingine anaweza kutumia ujumbe mfupi utakao fichua uovu wako?
3.     Je, umeshawahi kufuta meseji kwenye simu yako kwa kuogopa kugunduliwa na mpenzi wako?
4.     Je, umeshawahi kutumiwa picha ambazo unadhani zitamkasirisha mpenzi wako.
5.     Je, una mawasiliano na mtu mwingine ambae usingependa mpenzi wako ajue juu ya mawasiliano hayo?
Iwapo moja kati ya maswali hayo kwako umejibu “NDIYO” ni wakati wa kuangalia upya iwapo kweli unampenda mpenzi wako kwa moyo wote au la.Na kama unaona umemnyima uhuru anaohitaji kweli unampenda au unamytumia tu?
Utakuwa unamtesa mpenzi wako kwa kumkataza asishike simu yako kwani hata wewe mwenyewe unajua kuwa sio kitu rahisi kuishi katika hali ya wasiwasi.Ni wajibu wako kutengeneza mazingira ambayo yatamletea amani mpenzi wako  kwa kumpa uhuru wa kushika simu yako.
Hebu fikiria, mpenzi wako yuko bafuni na ameacha simu kitandani na mara unasikia meseji zinaingia mfululizo,kwa hali ya uanadamu unapatwa na hamu ya kutaka kujua kuna nani anayetuma meseji hizo. Dada mmoja aliamua kufanya utafiti miongoni mwa marafiki zake kwenye facebook na kuona kuwa wengi wanaliona hilo kuwa jambo baya lakini wengi wao wanasema bado wanajikuta wnachungulia kuona kuna nini kwenye simu za wapenzi wao bila ya kupewa ruhusa ya kufanya hivyo.Kwanini watu ambao wanasema sio vizuri kupekua simu za wapenzi wao wanajikuta wanashindwa kujizuia na kupekua simu hizo pale wanapoamini kuwa wapenzi wao hawawezi kugundua?WATU  HAO HUFANYA HIVYO KWNI NI HALI YA UANADAMU WETU KUTAFUTA  UHAKIKA WA MAMBO ili kuwa na amani.
Pale unapopewa uhuru wa kupekua simu ya mpenzi wako lazima uwe na uhakika kuwa unao uwezo wa kukabiliana na madudu ambayo unaweza kuyakuta yamezaliana kwenye simu ya mpenzi wako. Na usishangae utakapoonyesha kuwa umaumia kukuta madudu yenye sura zinazotisha na hapo hapo ukasikia mpenzi wako akisema “shauri yako umeyataka mwenyewe, usingepekuwa simu yangu hayo yote yasingekukuta na hata pole sikupi”.
Watu wengine wanaopigia debe haki ya kuheshimu uhuru wa mpenzi wako wanasema kuwa iwapo una wasiwasi na mpenzi wako badala ya kupekua simu yake mueleze juu ya wasiwasi huo. Ukweli ni kwamba unapomuuliza mpenzi wako upo uwezekano mkubwa wa kudanganywa kwa maneno na ni rahisi kupata ukweli kwa kupekua simu.
Pamoja na yote niliongea katika mada hii napenda nitoe thadhari. Uanzapo kuwa na uhuru wa kupekuwa simu utajikuta umekuwa aina fulani ya mlevi na huwezi kutulia mpaka umepekua simu yake jambo ambalo kwa mtu ambae sie muelewa anaweza kukuona kuwa ni mtu unaeboa na huna jambo jipya la kusisimua. Unapokuwa mlevi wa kupekua simu ya mpenzi wako utajikuta huna raha mpaka utakapomaliza kupekuwa jambo ambalo lina uwezo wa kupunguza uwezo wako wa kuonyesha mapenzi ambayo yatakufanya umpende zaidi.  Katika mazingira kama hayo utakuta unaharibu uhusiano badala ya kujenga. Dada mmoja alijikuta amekuwa mlevi wa kupekuwa simu za mpenzi wake na akaona hiyo haikutosha akaanza pia kupekua simu ya baba ya mzazi.Ni  jambo jema lakini lazima uwe na hekima  usije ukabomoa penzi  lenu.
Pamoja na hayo yote utajikuta unakosa raha kila unaposikia mlio wa meseji inayoingia katika simu ya mpenzi wako na hapo hapo unajikuta unatamani uikwapue simu yake uwe wa kwanza kuisoma meseji hiyo jambo ambalo litkufanya uwe huna raha mara kwa mara na hivyo kumboa mpenzi wako.
Kusema kwamba unapaswa kumuamini mpenzi wako na uache kupekuwa simu yake sio sahihi. Ili uweze kumuamini mtu lazima akupe ushahidi wa kutosha kuwa anastahili kuaminiwa. Kama kweli mpenzi wako anakupenda atakupa uhuru wa kupekua simu yake na pale unapoona  hukuti jambo lolote baya wewe mwenyewe utaona aibu na utalazimika kuacha labda pale ambapo kiwango cha penzi kimepungua sana kati yenu  na hujui sababu ya hali hiyo.
Pale uonapo mpenzi wako ana tabia ya kupekua simu yako jitahidi kuwa muelewa badala ya kuchukia. Iwapo huko nyuma aliamini mtu na mtu huyo alimsaliti anayo haki ya kujilinda asiumie tena. Wala sio hilo tu huenda rafiki yake wa karibu alishawahi kusalitiwa na mwanaume mwingine  baada ya kukuta meseji inayomsema vibaya kwa mtu mwingine.na akaumia sana. Hebu fikiria uwe na rafiki wako wa karibu sana akuletee mkasa uliomkuta baada ya kupekuwa simu ya mpenzi wake. Hebu sikia maneno kama haya “John usiamini wanawake bwana, unaweza kuamini kuwa awitness alikukwa anatembea na wanaume wawili kwa mpigo? Jumapili ametoka kwangu saa 8 mchana anasema anaenda discussion na wanafunzi wenzake na kesho yake nakuta meseji ya jana inayosema alienda NORTH HOTEL na mwanaume mwingine. Nilimwona  WITNESS mtu mpole sana na anaejiheshimu na nikamuamini sana lakini bada ya kusoma meseji hiyo niliumia sana na sijui kama nitaweza kumuamini mwanamke mwingine tena” itakuwa mbaya zaidi iwapo rafiki yako huyo atakusimulia mkasa huo huku akitoa machozi mengi na akakupa kazi ya kumfariji.
NDUGU yangu, jitahidi kutumia simu yako kumletea mpenzi wako furaha na sio wasiwasi.KWA kadri utakavudhamiria kutumia simu yako kujenga na kupamba penzi kwa kumpiga mpenzi wako, kutuma mesejei tamu za kimahaba   itakuwa vigumu kwako kufanya hayo kwa mtu mwingine tofauti .Wakati umefika wa wewe na mpezi wako kufanya bidii za makusudi kuongezea kiwango cha furaha na msisimko kati yenu kwa kutumia simu za mkononi.
Kabla ya kumaliza naomba nikusomee maneno ya dada mmoja yanayothibitisha umuhimu wa kupekuwa simu ya mpenzi wako.
“Nimejikuta kuwa nashindwa kuacha kupekua simu ya mpenzi wangu baada ya mwanaume wa kwanza maishani mwangu kunisaliti. Niligundua kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wawili tofauti, wakati tayari alikuwa amekwisha nitolea mahari. Natamani ningesema kuwa najuta kupekua simu yake lakini sijui hata kidogo. Sijuti kwa kuwa kama isingekuwa kwa kufanya hivyo ningeendelea kuamini kuwa mwaminifu kumbe yeye ananiona bwege kwa muda mrefu sana. Niliumia sana lakini nilijifunza somo moja muhimu sana . Kupekua simu ndio njia pekee ya kupata uhakika na majibu sahihi muda wangu ni wa muhimu sna na sitaki mwanume yeyote anipotezee muda wangu”.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages