Wanaume wengi huwa na maneno mengi mabaya,aina ya wanaume ambao hawafuati yafuatayo , hata hivyo kwa mwanaume ambaye hufuata taratibu nzuri za ukweli, wakati anapopata mtu huwa anajua kuwa ataishi nae maisha yake yote, atafanya kazi kwa bidii kwa ajiliya kuwaweka karibu yake muda wote, kama una mwanaume wa aina hio anayefanana na dalili hizi zifuatazo, ujue ni milinzi wa maisha yako.
1.Anajituma Kwa Ajili Yako Na Mahusiano yenu Pamoja.
Kuwa hapo muda wote ni rahisi sana, ila kuwepo pale kwa wakati mgumu ndio muhimu kushikana pamoja, mwanaume wa ukweli hakimbii matatizo, na huwa hawachukulie kirahisi pale mwenzake anapokuwa na hali mbaya hukaa bega kwa bega, wanaelewa umuhimu wa mahusiano ni nini, na hawaachi kitu chochote kiingilie kati.
2.Haepuki Matatizo.
Kama nilivyosema, mwanaume wa ukweli hakimbii pale mambo yanapokuwa magumu, na kuharibika, na pia haondoi hisia zake kwa mke wake hata kama kuna tatizo gani la kutoelewana mpaka arekebishe. Ama ikiwa limemsumbua ndani ya mahusiano yake huwa analileta kwa hekima , kwa uangalifu na kwa heshima. Anakuwa huru anapoongelea tatizo aliloliona , na anatafuta njia ya kulitatua. Anaelewa hata kama lina ukubwa gani haliwezi kuharibu mahusiano.hivi ndivyo afanyavyo.
3.Husikiliza Hata Vitu vidogo Tu.
Angekuwa anaishi peke yake , asingejali hata kama hakupata chakula kizuri, kwa sababu hakuna mtu wa kumpikia. Lakini anaelewa kuwa unamjali na kumpikia na kumfanyia vitu vingi ambavyo yeye wakati mwingine alikuwa hawezi, anaamua kutafuta muda wa kukusaidia kazi siku akiwa nyumbani, kama kupika na kufua na wakati mwingine kufanya hata usafi wa nyumba na anafurahia kufanya hivyo. Hatakaa tu kusoma gazeti na kuangalia Tv. wote mtafurahia kuwa pamoja kila mahali.na atakuachia simu yake uwe nayo upendavyo.
4.Ni mwenye Hekima na yuko smart.
Nitakupa faida za kuona kuwa umepata mwanaume smart. Lakini ukweli ndio unaompima mwanaume mwenye uwelewa na ufahamu jinsi alivyo makini, lakini anafanya kwa hekima yake. Huona kitu kwa kutazama hali ya mtu kwa muda huo,na yuko tayari kukushauri kwa hali yoyote ile unayopitia. Na hatakuacha usononeke, anavaa viatu vyako ili aone ni wapi unapoumia, na anawaambia watoto wako maneno ya hekima ya kuwatuliza endapo kulikuwepo tatizo.
5.Anataka Ujisikie Vizuri Kila wakati.
Huwa anafikiria kuwa wewe ni mzuri ,kwa nini awe na wewe kama hataweza? Lakini haitoshi kufikiria yeye kufikiria hivyo, pia hufanya zaidi ili ujitambue kuwa wewe ni mzuri, wala sio kwa maneno ya kawaida ya kumhakikishia, hata pale unapokuwa na hali mbaya anahakikisha uko vizuri, atakuja na njia za kukufanya ujisikie vizuri ndani na nje, kutokana na hali uliokuwa nayo kwa muda huo. Atafanya vyovyote awezavyo ilin uelewe kuwa anakuona kila kitu na kila siku.
6.Anabeba Shida zako Kama Zake.
Kama kuna kitu kinakusumbua, kitamsumbua nae pia, atachukua hayo matatizo na kujaribu kuyatatua au kuondoa maumivu yake kiasi awezavyo. Shida zako humweka macho usiku, na wala haimsumbui,kinachomsumbua yeye ni kwa nini hawezi kutatua tatizo lililopo mbele yako. Hali hii inapokuja hujitahidi kusimama nalo haijalishi lina ugumu gani.
7.Hucheka Unapokosea.
Anaelewa kila mtu hufanya ma.kosa, na yuko tayari muda wowote kulitatua kwa urahisi, ukisema kitu kinachomuudhi, anaamini hukuwa na maana hio, yeye hucheka hata kama wewe ulimaansha kidogo. Ukimwangusha, kwa mfano alikuwa anatarajia uwahi nyumbani kwa ajili yake, hawezi kushikilia hicho kitu atasamehe mara moja. Hujali na ni sensitive. Hatakufanya ujisikie vibaya kwa sababu ataumiza hisia zake.
8.Huwa mwangalifu na makosa yake.
Kwa upande mwingine, chochote kinachokuumiza atakipima na kukibeba mabegani mwake kwa muda huanza kujipiga mwenyewe kuhusia na hilo , lakini anapokusababishia wewe maumivu, atafanya kila njia ya kujirekebisha hatakuambia jambo lolote ili kukuweka sawa kwa unafiki, au aseme kuwa alikuwa anadanganya, anakuelewa vizuri, anafahamu kabisa kitu gani amefanya kukudhuru , lakini hataweza kamwe kwenye ndoto ya miaka milioni namna hio.
No comments:
Post a Comment