Nilikutana na mume wangu wakwanza kipindi nina miaka 26, yeye alikua na miaka 30, kipindi hicho alikua hana kazi na mimi nilikua nafanya biashara ndogo ndgogo, tulipendana na kuamua kuishi pamoja, nilimtafutia biashara za kufanya na kweli alikua anafanikiwa lakini tatizo alikua ni mlevi. Alikua anakunywa pombe sana kiasi cha kujisahau, pesa yote ilikua inaishia kwenye pombe mpaka ikafikia wakari ananiibia, alikua akilala nnje kila siku napigiwa simu kuwa niende kumchukua.
Nilihangaika sana kwenye maombi na kila sehemu kwani nilihisi labda kuna watu wanamfanyia hivyo lakini hakubadilika. Nililazimika kuachana naye kwani alikua hakai nyumbani, hajali familia na kila siku ikawa nikilalamika ni kipigo. Alinizalisha watoto wanne lakini nao alikua hahudumii kowa chochote, nililazimika kuondoka na kwenda kupanga sehemu nyingine, kodi ilipoisha aliondoka kabisa na mpaka sasa hivi hata sijui yuko wapi?
Hahudumii watoto, hapigi simu wala kujali kwa chochote, ni miaka mitano sasa tangu naichane naye lakini hajawahi hata kutuma Shilingi kumi au kupiga simu kujua kama watoto wake wanaendeleaje. Kwakua mimi ni mpambanaji niliamua kuendelea na maisha yangu, nilikaa miaka miwili bila mwanaume, mwaka 2016 nilikutana na kijana mwingine, yeye alikua akiishi kwa Kaka yake na alikua hana kazi, tulipendana na kwakua sikua na mtu nikaamua kuingia naye kwenye mahusiano.
Baada ya kuingia naye kwenye mahusiano aliniambia kuwa ana mwanamke ambaye aliazaa naye watoto watatu, hawakufunga ndoa lakini bado wanawasiliana kimapenzi ingawa mwanamke anaishi kwao na hajamchukua kwakua hana sehemu ya kumuweka. Mimi sikuona shida, nilimchukua mwanaume na kuanza kuishi naye kwangu, kwakua hakua na kazi na mimi nilikua nafanya Biashara nilimuingiza katika Biashara zangu tukawa tunafanya pamoja, mimi nafanya Biashara ya nafaka, nanunua mpunga, maharage na mahindi na tayari nilishatengeneza jina.
Tulifanya naye ile Biashara kwa mwaka mmoja, tatizo likaja kwa yule wmanamke wake, alikua anasumbua sana hasa matumizi, kila wakati kupiga simu hivyo mwanaume hakua na amanai. Nilimshauri mwanaume kumchukua mwanamke na kumleta Dar ili wote tuwa tunaishi mjini na aasisumbuke kuhudumia, alimchukua kweli akaja kumpangishia nyumba yeye na wanae watatu, tukawa tunaishi vizuri tu, mimi naishi kwangu na wanangu wa nne ambao nilizaa na mwanaume wangu wakwanza na yule mwanamke mwingine anaishi kwake lakini kila kitu nikilipa mimi.
Baada ya kuona familia imekua kubwa niliamua mimi kufungua Biashara nyingine na kumuachia mume wangu ile Biashara ya nafaka ili aisimamie kwani alishaijulia. Nilienda sokoni na kufungua Biashara ya nguo, niakwa nauza mtumba, nakata beli nauza kwa jumla na rejareja. Mwaka huu mwanzoni nilipata ujauzito wa mume wangu, kutokana na mishemishe na mimba kusumbua nililazimika kuacha ile Biashara nakubaki tu nyumbani, tukawa tunamtegemea mwanaume kwa kila kitu wote wawili.
Hapo ndiyo nilianza kuona mambo magumu, kumbe mwanaume alikua na mwanamke mwingine ambaye ndiyo walianza naye maisha na kuzaa mtoto mmoja kabla ya kuktana na huyu mwingine. Alimchukua mtoto na kumleta hapa nyumbani, akamchukua mwanamke mwingine na kumpangishia chumba, nilikasitika kwani alinidanganya lakini alikataa katakakata kumuacha akisema kuwa huyo ndyo mwanamke wake wa kwanza alianza naye maisha hivyo hawezi kuachana naye.
Ilikua shida sana kwangu kukubali lakini niliamua kuvumilia kwakua nampena nayeye alinihakikishia ananipenda hataniacha. Tatizo mpaka kuja kuomba ushauri nikuwa Biashara imekufa, mimi ndiyo nimetoka kujifungua lakini mwanaume kaua Biashara yangu, kala mtaji wote na hana hata Shilingi kumi. Amekua ni mtu wa kukaa nyumbani na hajali. Kumguka hapo kuna watoto sita, wanne nilizaa kabla ya yeye, mmoja mimi na yeye ambaye ana mwezi sasa na mwingine ni ambaye alizaa na mwanamke wake wa kwanza.
Lakini kule kwingine kuna mwanamke mwingine na watoto watatu na wote wanamtegemea yeye ila hajishughulishi kwa chochote na haonyeshi kujali. Kama mwanamke nililazimika kutoka na kwakua nafahamiana na watu nimekua nikikopa mzigo nauza nikipata vie elfu kumi ndiyo tunakula maisha yanasogea. Tatizo nikuwa yule mwanamke mwingine hajishughulishi kwa chochote na mwanaume naye hata hajikuni, kwahiyo nikipata elfu kumi anataka tugawane ili atoe na kule watoto wasife njaa.
Mimi bado nampenda na nahofia nikiachana naye watu watasemaje kwani atakua ni mwanaume wangu wa pil! Nitapata wapi mwanaume mwingine wakunioa kwa umri wangu huu wa miaka 36 na watoto wa tano tena wa Baba wawili tofauti. Nimechanganyikiwa Kaka naomba msaada wako, niambie nakosea wpi na nifanye nini ili huyu mwanume aweze kunisaidia kulea familia. Ndiyo nimetoka uzazi mwezi mmoja tu, bado sina nguvu, nalazimika kumuacha mtoto nyumbani kwenda kuhangaika kutafuta wakati mwanaume kakaa ndani ana nikirudi anataka nimpe pesa kwaajili ya familia yake nyingine, nimekwama sijui nifanye nini Kaka!
Kibaya zaidi Kaka nimekuja kugundua kuwa kumbe huyu mwanaume kule dukani kwangu alikokufilizi kuna mwanamke alikua anatembea naye na sasa hivia na mimba yake. Nimemuuliza amekiri na kuniomba samahani anasema kuwa ni bahati mabya alipitiwa kipindi mimi nina ujauzito, nashindwa kuelewa Kaka ni bahati mbaya kweli kwani ana wanawake wawili na pia na hisi yule wa kwanza bado wana mahusiano ya kimapenzi ila kashindwa kuvumilia kaenda kuzaa na mwanamke mwingine, je huyu mtu ni sahihi kwangu Kaka? Nifanyeje ili abadilike na mimi kuwa na amani kama wanawake wengine?
***,MWISHO
No comments:
Post a Comment