Zipime tabia za mtu wakati mko kwenye uchumba halafu ukijiridhisha ndio useme sasa nataka kuingia kwenye ndoa,,,
Amini kama kwenye uchumba sehemu ambayo mtu anaweza kufanya mambo mengi ili akushawishi kutaka ndoa,,umeona kuna vitu umetaka abadilike akashindwa wala usijiaminishe kuwa ukiingia kwenye ndoa atabadilika tena usishangae tabia hiyo ndo ikazidi,,
Pambana sana either kuzibadilisha tabia za mpenzi wako au kuzizoea tabia za mpenzi wako,,,kumfanya ajue nini unapenda na nini hupendi ajue mapema kabla ya siku yako ya ndoa ili ukiona vimeshindikana basi hiyo ndoa achana nayo maana unaenda kukaribisha machozi na mateso tu,,
Usiingie kwenye ndoa kwa imani kwamba baada ya ndoa atabadilika,,,akishindwa kubadilika kwenye uchumba achana nae.
No comments:
Post a Comment