DADA HUYU NDIYE MWANAUME BORA - Utundu kitandani

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2019

DADA HUYU NDIYE MWANAUME BORA


1.Anakujali,,anakupigia simu mara kwa mara kukuuliza siku yako imeendaje,,anafanya hivi kirafiki na kwa upendo,, haigizi,,anakupenda kweli.

2.Anakutembelea mara kwa mara,, anakuwa na wewe karibu wakati unaumwa,,hii inamaanisha yupo tayari kukuvumilia kwenye shida na raha,,mpende mwanaume huyu.

3.Anawapenda ndugu kama ndugu zake,,,anaongea nao vizuri ns kusaidiana mambo ya hapa na pale,,mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume.

4.Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole,,anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenda ndivyo sivyo,,anakuelekeza njia zilizonyooka,,usimwache huyu mwanaume

5.hakulazimishi kufanya mapenzi,,anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo,,yupo karibu na wewe muda wote na sio tu anapokuwa anakutaka kimapenzi,,huyu ni bonge la bwana.

6.Anakusaidia fedha na ushauri pale unapokuwa umekwama kabisa,,yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi,,anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho,,hana mkono wa birika,anakupenda

7.Anazungumzia future yake na wewe,,mipango ya baadae pamoja na wewe,,,huyo ana dhamira ya DHATI toka moyoni mwake ya kukufanya kuwa mkewe

Hizi ni moja ya dalili ya kwamba mwanaume huyu anakupenda na anataka kutengeneza future na wewe,,,usikate tamaa juu ya aina hii ya mwanaume.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages